Ndoa ya @mcpilipili ni batili kutokana na kwenda kinyume na kiapo cha ndoa”

Acha basi! Kwahiyo itarudiwa au!

Baba Akofu Wiliam Mwamalanga amefunguka na kudai kuwa ndoa iliyofanyiaka siku ya jumamosi ikimuhusisha mchekeshaji na mshereheshaji Mc Pilipili na mke wake Philemona kuwa ni batili.Mchekeshaji MC Pilipili na mpenzi wake Philomena, siku ya jumamosi iliyopita ya tarehe 29/7, walifunga pingu za maisha katika kanisa la Mbezi Chapel jijini Dar es Salaam na kuhitimisha a very long wedding promo ever in Tanzania.Licha ya kuwa harusi iliyotrend vyema mtandaoni na pia kuonyeshwa kwenye kituo cha luninga, ndoa hiyo ilizua minong’ono sana mitandaoni baada ya wawili hao wakati wa ufungaishaji wa ndoa hiyo waliibuka na viapo vyao vilivyo tofauti na vilivyozoeleka.

Cheki a video hii hapa;

 
Wakati wa ufungaji wa ndoa hiyo kwenye lile eneo la kula kiapo badala ya kusema katika shida na raha yeye aliongezea neno lake na kuwa atampenda mke wake nyakati za baraka zaidi.
licha ya makelele mengi mtandaoni, hili limemuibua Baba Askofu Wiliam Mwamalanga na kuamua kilitolea ufafanuzi suala hili. Baba Askofu anadai kuwa kiapo hicho hakikuwa halali na kwamba kipo kiapo maalumu ambacho kinatumika katika kanisa na ndicho kinachotambulika.Kama unakiapo chako ni vizuri kukipeleka sehemu yako hata bichi, lakini kama ukiingia kwenye nyumba ya ibada ni muhimu kufuata kiapo cha sehemu husika na sio kubadilisha, huenda wengine wakaona ni jambo la kawaida lakini hakuna mzaha kwenye neno la Mungu hata biblia inasema tusikaribie kwenye meza ya mizaha”
Je kama kiapo ni haramu na ndoa vipi Baba Askofu?Ni nini Mc Pilipili anaambia watu?

Akijitetea juu ya alichokifanya, Mc Pilipili amedai kuwa alimaanisha kuwa hakutaka kukaribisha magonjwa au njaa katika ndoa yake

“Sikuwa namaanisha vibaya pale kanisani wakati nasema kiapo changu cha ndoa, dhumuni langu lilikuwa ni kutokaribisha magonjwa au njaa kwenye ndoa yangu na sikuwa na lengo bayaBaadhi ya wadau wamedai kuwa Mc Pilipili hakukosea kwani hakuna mstari kwenye kitabu cha dini kilichoweka mstari huo;,
Je wewe mawazo ni yapi?, toa hapa

No comments