Wabunge wa Wapinzani walitaka KKKT kutojibu barua ya Serikali

WABUNGE wa Upinzani Bungeni wamewataka viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki (RC) kutoijibu serikali kuhusu barua waliyopewa na Msajili wa Vyama akiwataka kukanusha waraka wao wa Kwaresma na Pasaka.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia akizugumza na wanahabari kwa niaba ya kambi hiyo leo Bungeni jijiji Dodoma, amesema mamlaka za nyaraka za makanisa hayo ni mamlaka ya kibiblia na kwamba makanisa hayo makubwa nchini yamekuwa yakitoa huduma kubwa ya kiroho kwenye jamii hivyo kwa jambo lililofanywa na msajili wa vyama wamedharauliwa.
“Naomba niseme kwamba, tunawashauri viongozi wa dini kutowajibu serikali, halafu tuone wanachukua hatua zipi,” amesema.
Mbunge wa Kibamba (Chadema) na Nanibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Bara, John Mnyika ameitaka serikali kukanusha barua hiyo na kwamba watatumia kanuni za bunge kwa siku 10 kuomba miongozo hadi serikali itakapotoa majibu ya jambo hilo.
“Hapa Naibu Spika (Tulia Akson) ametumia madaraka vibaya akimkingia kifua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asijibu jambo hili bungeni, ndani ya siku 10 sisi tutauliza maswali, tutaomba miongozo hadi serikali iwajibike, tutafanya kwa umoja wetu hadi haki ya viongozi hawa wa dini ipatikane,” amesema Mnyika.
Jana Barua ilisambaa kwenye vyombo vya habari ikieleza kuwa Msajili wa Vyama nchini amezitaka Kanisa la KKT na Kanisa Katoliki kufuta waraka wao wa Pasaka na Kwaresma kwa serikali huku akimtaka Askofu Mkuu wa KKKT kufika ofisini hapo kuchukua malimbikizo ya madeni wanayodaiwa na wayalipe ndani ya siku saba.
Leo Juni 7, 2018 Mbatia alimuuliza swali Bungeni Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitaka kusikia kauli ya serikali kuhusu kuwataka viongozi hao wa dini kufuta walaka huop. Hata hivyo Spika wa bunge alikataa na kusema swali hilo haliwezi kujibiwa Bungeni na Waziri Mkuu.
Sakata Waraka-: KKKT, Kanisa katoliki, Msijibu Barua ya Msajiri – Mbatia
Post a Comment