'Ni marufuku kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa'Paroko wa Katoliki alisema
Arusha-Tanzania
-
Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padri Festus Mangwangi, alisema hayo jana akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita
-
Askofu Amani alisema wazazi wanatakiwa kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo alama ya shela itakapoonekana umuhimu wake
-
Padri Mangwangi alisema atakayedanganya na kuvaa shela wakati tayari anamjua mwanamume au ni mjamzito atakuwa anafanya utovu wa nidhamu,kwani sio sahihi kufanya hivyo!
Post a Comment