Ghafla mastaa hawa wa Tz(bongo) walimgeukia Mungu,je ni kwanini

SUALA la wasanii na watu maarufu kutangaza kuacha maovu na kumrudia muumba wao si geni. Kwa hapa Bongo wapo wengi ambao wamewahi kufanya hivyo,na ukiangalia wasanii wengi wamejitokeza kuokoka.
Wapo ambao huweza kudumu katika wokovu huo na wapo wengine ambao shetani huwavuta shati na kujikuta wakirudi kwenye himaya yake. Matukio yote hayo yanasogeza siku za maisha mbele!
Sasa ukiangalia katika suala la kuokoa na kuwa smart,tofauti na baadhi ya watu wengi wakiokoka huwa wanaacha kila kitu hadi mapambo na hasa kwa wanawake.
Mwanaspoti linakuletea wasanii watatu waliokoka na bado wako smart,wenyewe katika suala la wokovu wanasema wametu yale ambayo walikuwa wanayafanya na kuona hayamlendezi Mungu ila katika suala la kukijiremba huwa haingiliani na Imani yao ya wokovu.
Blandina Chagula ‘Johari’
Ni muigizaji wa Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amedai kubadili mfumo wa maisha yake na kuahidi kuokoka ili kujiweka karibu na Mungu, ikiwa ni pamoja na kuachana na maisha ya ajabu kama matumizi ya pombe.
Johari aliliambia Mwanaspoti kuwa, amebaini maisha ni mafupi duniani hivyo ni vyema kujisafishia njia na kumrudia Mungu ambaye ndiye mwokozi wa maisha ya wanadamu.
“Ninaachana kabisa na mambo ya kidunia, sitaki tena pombe wala kujihusisha na maisha mengine yenye kumchukiza Mungu, nimefanya mambo mengi yasiyokuwa mazuri. Kama binadamu, ninajipanga kuwa mpya na ninasema kabisa kwamba nimeokoka,” alisema Johari.
Kajala ni mwigizaji wa filamu za kibongo,alitangaza ameokoka na kuamua kumrudia Mungu kwa sababu ameona mambo ya kidunia kwa wakati huu hayana nafasi na sio ya kuyaendekeza.
Alisema kwa kukiri kuwa,tangu aokoke a mambo yake mengi yamekuwa yakigunguliwa ikiwa pamoja na kujitambua .
“Nimeamua kwa akili yangu mwenyewe kurudi kwa Muumba wangu kwa sababu haya mambo ya kidunia yana mwisho wake na hata mastaa wenzangu wanapaswa kumuabudu Mungu hata kwa juma mara moja kwa maana chochote walicho nacho ni kwa ajili ya yeye,”alisema Kajala
Lulu ni Muigizaji wa filamu nchini,yeye aliwahi sema ameokoka baada ya kupata misukosuko ya kimaisha,ndio akaamua maisha yake ayaelekezew katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake.
“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,ila cha msingi nashukuru nimeacha matendo mabovu na kuwa mtu mpya wa mungu,” aliwahi sema Lulu
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
Ni msanii wa filamu za kibongo,yeye amesema ameamua kuokoka baada ya kuamua kubadiri mfumo wa maisha yake,aliyokuwa akiishi zamani baada ya kuendekeza starehe.
Amesema amemrudia Mungu hivyo muda mwingi anashinda ndani akiwa anasoma biblia sababu kaona mungu ndio rafiki wa kweli.
Post a Comment