UUVCCM KUJIPANGA NA UCHAGUZI 2025


 Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Jokate Mwegelo amesema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji pamoja na uchaguzi mkuu wa 2025 vijana wamejipanga kuhakikisha wanapambana mitandaoni na majukwaani ili chama hicho kiendelee kupata viongozi sahihi.

Jokate amesema hayo wakati wa mapokezi katika ofisi za makao makuu ya chama cha Mapinduzi CCM jijini Dodoma ambapo leo wamepokelewa viongozi walioteuliwa hivi karibuni akiwemo Naibu Katibu Mkuu bara John Mongela,Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Taifa Ally Hapi,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Jakate Mwegelo na Katibu wa Siasa,Itikadi,Uenezi na Mafunzo Amos Makala

“Wanaosubiri vijana wa chama cha mapinduzi wakosee watasubiri sana vijana tupo imara na tupo timamu na tupo tayari kwa kazi ngumu na nyepesi kwa mwaka huu na mwaka 2025 na tutazisaka kura popote ndani ya Tanzania iwe bara iwe visiwani pengine kuna watu hakuelewa tutazisaka vipi hizo kura ilani njema ya chama cha mapinduzi imetuwezesha tumepata elimu tumeelimika na tumejiendeleza na tunataknolojia tutawapiga mtandaoni na tutawapiga mtaani na tutwajibu kwa hoja sio brabraa” Jokate Mwegelo katibu Mkuu UVCCM

No comments