Deni la Serikali ni TRIL. 82.25


 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, leo amewasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyazungumzia ni deni la Taifa.


“Kufikia June 30,2023 deni la Serikali lilikuwa Tsh. trilioni 82.25 sawa na ongezeko la 15% kutoka Tsh.trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/2022, deni hilo linajumuisha deni la ndani Tsh. trilioni 28.92 na deni la nje Tsh. trilioni 53.32 kipimo kinaonesha deni hili ni himilivu”


“Uwiano wa kulipa madeni na mauzo ya nje ni 12.7% chini kidogo ya kiwango cha ukomo cha 15% na uwiano wa malipo ya madeni na mapato ni 14.3% chini kidogo ya kiwango cha ukomo elekezi cha 18%” ——— Kichere. 


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere leo amewasilisha Ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyasema kwenye ripoti hiyo ni kuhusu Bilioni 6 ambazo zilikusanywa na Halmashauri lakini hazikuwasilishwa Benki.


“Ukaguzi umebaini kuwa Halmashauri hazikukusanya Tsh. bilioni 61.15 kutoka katika vyanzo muhimu na vikubwa wakati Tsh. bilioni 6.19 zilizokusanywa hazikuwasilishwa Benki”


“Hali hii inaathiri uwezo wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa Jamii” amesema CAG Kichere. 


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere leo amewasilisha Ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Dodoma ambapo moja ya aliyoyasema kwenye ripoti hiyo ni kuhusu Mashirika nane kukusanya pesa nje ya mfumo wa malipo ya Serikali.


“Nilibaini kuwa Mashirika 8 ya Umma yalikusanya mapato ya Tsh. bilioni 23.27 nje ya mfumo wa kielektroniki wa malipo ya Serikali (GePG) kinyume na waraka wa hazina namba 3 wa mwaka 2017, kushindwa kukusanya mapato kupitia GePG kunaweza kusababisha upotevu wa mapato na kufifisha juhudi za udhibiti na uwazi katika mapato ya Serikali” ——— Kichere. 

 #RipotiyaCAGMarch2024

No comments