Je Yanga atafuzu hatua ya makundi? ⚽️


 ⚽️ TOTAL DOMINANCE ( FT: Yanga SC 3-0 Medeama )


✍🏻Yani kama ingekuwa mchezo wa Boxing basi tungesema Medeama hata punch moja haikufika kwenye uso wa Yanga. Yanga walikuwa bora kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho na kwa aina ya nafasi ambazo walitengeneza 3-0 ni matokeo yanayodanganya 


✍🏻Msingi mkubwa wa Yanga ulikuwa hapa kwenye positions za hawa wachezaji wawili pale Yanga wakiwa na mali : Kibabage na Mudathir . Maeneo ambayo walikuwa wanasimama/ wanakuwa hayo maeneo ndio msingi mkubwa . 


1: Kibabage anasogea juu zaidi ya uwanja kama winga na Mudthir anatoka ndani na kwenda pembeni kuwa kama winga wa kulia . Ilikuwa na faida gani ? 


2: Ni kuruhusu viungo watatu washambuliaji kucheza katikati ya mstari wa kiungo na ulinzi wa Medeama tunaita " between the lines " ( Aziz , Maxi na Pacome ) ndio sehemu ambazo walikuwa wanapokelea mipira na ilikuwa hatari sana kwa Medeama na ngumu kwao kukabiliana nayo .... faida yake ? 


3: Kuwa na wachezaji wako hatari katika maeneo hatari na magumu kuzuia , maana yake wana options hizi : Kupiga golini na kupiga pasi za mwisho kwa Kibabage Musonda Mudathir na pia kwao wao wenyewe kwa wenyewe 


4: Lakini wao kuwa eneo hilo kitu kimoja na kupata pasi sahihi kwa wakati sahihi ni kitu kingine . Hapo ndio anaingia kiungo mwenye kazi hiyo : Aucho . Anajua sana kupiga pasi za mbele tena za chini chini ambazo zinavunja mstari wa kiungo wa timu pinzani ( Line breaking passes ) 


✍🏻Nafikiri Medeama ni kama vile walikosa imani kwamba wanaweza kuonesha mamlaka uwanjani na haiba ya kuutaka mchezo , walikuwa slow sana , mipira wanapoteza kirahisi ( kama kwenye goli la tatu la Yanga ) wanachelewa kufika kwenye mpira , recovery runs zilikuwa za chini sana na ukicheza dhidi ya wachezaji wazuri watakupa shida sana . 



NOTE 


1: Gamondi alikochi ushindi wa 6-0 lakini wachezaji wameamua kumpa 3-0 . 


2: Yao Yao , Mr. Reliable . Performance zake ni nzuri kila ukimuona uwanjani 


3: Job na Bakari walifanya homework yao dhidi ya Sowah , leo walikuwa vizuri tofauti na Ghana 


4: Pasi za mbele za Aucho ndio msingi kwa Maxi Pacome na Aziz 


5: PACOME .. what a player . He is so good 🔥🔥


CC George Ambangile.. Toa maoni yako, Yanga atafuzu hatua ya makundi au hapana? ⚽️ 🔥 

No comments