SAJILI ZILIZOFELI SIMBA HADI SASA
🇹🇿| Kuna wakati wa kusajili halafu kuna wakati wakukitumia kile ambacho umekisajili.
Simba msimu huu imesajili wachezaji Wengi ambao baadaye wameonekana kushindwa chini ya kocha Robertihno Olveira.
Leandre Willy Essomba Onana aliimbwa saana wakati wakusajiliwa lakini mambo yamemwendea ndivyo sivyo, mpaka sasa akiwa na goli moja NBC Premiere League, Alionekana kuaminiwa na kocha michezo ya mwanzoni lakini baadaye alitolewa kwenye kikosi.
Iddi Shabani Chilunda, Huyu hajapata nafasi ya kucheza, hajaanza kwenye mchezo wowote Miaka (25),anatakiwa kupambana kupata nafasi yake katiko kikosi cha Kwanza.
Aubin Kramo! Yeye anapona majeraha na anaumia kwenye mechi za Mazoezi maheruhi yanamwandama saana.
Ayoub Lakred, mechi zote alizocheza tiyari ameruhusu magoli.
Kazi ipo!??

Post a Comment