Vita: Griezmann klabuni Atletico


  Kwa mujibu wa habari, Barcelona wanaandaa kesi dhidi ya Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa Antoine Griezmann, na watadai kipengele cha ununuzi cha €40m mara moja. 


Barca wanaamini na wanahisi kabisa mshambuliaji huyo tayari amecheza dakika za kutosha ndani ya kikosi cha Atl Madrid na anapaswa kuwa mchezaji wao wa kudumu. Ikiwa Griezmann alicheza 50% ya michezo katika mwaka wa 1, Atleti italazimika kulipa €40M na kumpata kabisa. Ikiwa sivyo, mkopo huo utasainiwa upya kuendelea kusalia kwa msimu wa pili. 


Hata hivyo, klabu hiyo inabishana kwamba Griezmann alicheza zaidi ya 50% msimu uliopita, ndiyo sababu Barcelona wanaamini kwamba masharti tayari yametimizwa na hivyo wanaidaiwa Atl. Madrid kiasi cha €40M. 


KWANI ATL. MADRID WAO WANASEMAJE? 


Alt. wao  wanakanusha taarifa ambazo zimetolewa kuhusu Griezmann na kipengele cha €40m. Atletico wanasema kwamba mkataba wa mchezaji huyo unaonyesha kwamba lazima acheze 50% ya michezo, ikizingatiwa kwa misimu miwili, sio msimu mmoja.



No comments