MAYELE ANUKIA BERKANE

Mabosi wa Yanga wanakuna kichwa baada ya Waarabu wa RS Berkane ya Morocco 🇲🇦 kutuma ofa nono, ili kumnyakua Fiston Mayele 🇨🇩 ambaye bado wanahitaji huduma yake huku naye akiwapa masharti mazito ili kusalia kikosini.
.
Berkane inayonolewa na kocha wa zamani wa AS Vita, Florent Ibenge, inamhitaji straika huyo ili kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao wa michuano.
.
Taarifa za ndani kutoka Yanga, Mayele ameuambia uongozi ili aweze kuendelea kubaki Jangwani ni lazima aongezewe mkataba na marupurupu kwenye mshahara wake wa sasa. Mayele kwa sasa ana mkataba uliosaliwa na mwaka mmoja.
TANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU, TUPIGIE 0679663340

No comments