Simba imeomba ulinzi wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Afrika kusini

Klabu ya Simba imeomba ulinzi wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Afrika kusini wakiwa safarini na wakifika nchini South Africa 🇿🇦 kwenye Mchezo wa Marudiano Shirikisho (CAF) dhidi ya Orlando Pirates.
.
.
Klabu hiyo imeeleza kuwa, vitisho visivyo vya moja kwa moja vilivyotolewa na kocha wa Orlando Pirates havipaswi kupuuzwa ndio maana wanaomba ulinzi katika kipindi chote klabu hiyo itakapokuwa nchini South Africa.
.
.
Pia klabu ya Simba sc imeeleza inapeleka malalamiko (CAF) na kwa balozi zote mbili yaani Tanzania na South Africa 🇿🇦 kuhusu shutuma walizopewa na kocha wa Orlando. 


No comments