AMKA NA BWANA LEO 05/01/2022
JUMATANO, JANUARI 5 2022
KUWA NA ROHO YA MSAMAHA
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mathayo 6:14, 15.
⏯ Mwokozi wetu aliwafundisha wanafunzi wake kuomba: "Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe wanaotukosea." Hapa, baraka kubwa inaombwa kwa masharti, na sisi wenyewe tunayatamka masharti hayo. Tunaomba kwamba rehema za Mungu kwetu zipimwe kulingana na rehema ambayo tunatoa kwa wengine. Kristo anatamka kuwa hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Bwana atashughulika nasi. "Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu." Sharti la pekee kabisa! Lakini ni kwa kiasi kidogo jinsi gani haya yanaeleweka na kufanyiwa kazi.
⏯ Moja ya dhambi za kawaida sana, na inakuwa na matokeo mabaya zaidi, kuendekezwa kwa roho ya kutokusamehe. Ni wangapi watakaothamini uhasama au kulipiza kisasi na kisha kuinama mbele za Mungu wakiomba kusamehewa kama wanavyosamehe. Kwa kweli hawawezi kuwa ufahamu wa kweli wa umuhimu wa ombi hili vinginevyo wasingethubutu kulitamka katika midomo yao. Tu wategemezi katika rehema inayosamehe ya Mungu kila siku na kila saa; tunawezaje basi kulea uchungu na ubaya kwa wenzetu wenye dhambi! Ikiwa, katika mahusiano yao yote ya kila siku, Wakristo wangedhihirisha kanuni za ombi hili, badiliko kubwa kiasi gani lingefanyika kanisani na duniani! Huu ungekuwa ni ushuhuda unaoshawishi sana ambao ungetolewa kuhusu uhalisia wa dini ya Biblia.
⏯ Tunaaswa na mtume: "Pendo lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu; mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu." Paulo anatutaka tutofautishe kati ya upendo safi, usio na ubinafsi unaochochewa na roho wa Kristo, na udanganyifu usio na maana ambao ulimwengu umejazwa nawo. Msingi huu wa bandia umepotosha roho nyingi. Utafutilia mbali utofautishaji kati ya haki na kosa, kwa kukubaliana na wakosaji badala ya kuwaonesha makosa yao kwa uaminifu. Jambo hili kamwe halitokei kwa urafiki kweli. Roho inayoongoza hili hukaa tu katika moyo wa kidunia.
🔘 Wakati Wakristo wakidumu kuwa wema, wenye huruma, na wenye kusamehe, hawawezi kuhisi maelewano na dhambi. Watachukizwa sana na uovu na kushikamana na kile kilicho chema, kwa kujinyima kufanya ushirika au urafiki na watu wasio wa Mungu. Roho ya Kristo itatuongoza kuichukia dhambi, wakati tukiwa tayari kujitolea kwa kila kitu kumwokoa mwenye dhambi.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment