AMKA NA BWANA LEO 03/01/2022

JUMATATU, JANUARI 3 2022

KUMKARIBIA MUNGU KWA UNYENYEKEVU 

Akawaambia, "Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], jina lako litakaswe, Ufalme wako uje. " Luka 11:2. 

📚 Kulitakasa jina la Bwana kunahitajika kuwa maneno tunayoongea kumhusu Mungu yatamkwe kwa unyenyekevu. "Jina lake ni takatifu la kuogopwa" (Zaburi 111:9). Hatupaswi kamwe kwa njia yoyote kuvichukulia kwa urahisi vyeo au majina ya Mwenyezi Mungu. Katika maombi tunaingia kwenye chumba cha hadhira cha Aliye Juu; tunapaswa kuja mbele zake kwa hofu takatifu. Malaika wanafunika nyuso zao mbele Zake. Makerubi na maserafi angavu na watakatifu wanakiendea kiti Chake cha enzi kwa heshima kubwa. Je! Si zaidi sana sisi, tulio na ukomo, viumbe wenye dhambi, kuja katika hali ya unyenyekevu mbele za Bwana, Mwumbaji wetu!

📚 Lakini kulitakasa jina la Bwana kuna maana kubwa zaidi ya hii. Tunaweza, kama Wayahudi katika nyakati za Kristo kudhihirisha heshima kuu ya nje kwa Mungu, na bado tukiendelea kulitusi jina Lake. "Jina la Bwana” ni Lake Aliye "mwingi wa huruma na mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli... mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi" (Kutoka 34:5-7). Kwa kanisa la Kristo imeandikwa, “Na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu" (Yeremia 33:16). Jina hili limewekwa juu ya kila mfuasi wa Kristo. Ni urithi wa mtoto wa Mungu. Familia zinaitwa kwa jina la Baba. Nabii Yeremia, katika wakati wa huzuni kuu na taabu, aliomba, “Tunaitwa kwa jina lako; usituache" (Yeremia 14:9).

🔘 Jina hili huwa linatakaswa au kutukuzwa na malaika wa mbinguni, na wakazi wa ulimwengu usioanguka. Wakati unapoomba, "Jina lako litukuzwe," unaomba kwamba liweze kutukuzwa katika dunia hii, na litukuzwe ndani yako. Mungu amekutambua wewe mbele za wanadamu na malaika kama mtoto Wake; omba kwamba usije ukaliaibisha "Jina lile zuri mliloitwa" (Yakobo 2:7). Mungu anakutuma duniani kama mwakilishi Wake. Katika kila kazi ya maisha unapaswa kulidhihirisha jina la Mungu. Ombi hili linakutaka uwe na tabia Yake. Huwezi kulitukuza jina Lake, huwezi kumwakilisha ulimwenguni, isipokuwa katika maisha na tabia unawakilisha maisha halisi na tabia ya Mungu. Hili unaweza kulifanya tu kupitia ukubali wa neema na haki ya Kristo.
===================
*Usikose Nakala ya Masomo ya Kesha La Asubuhi: Kuwa Kama Yesu, Seh. 1*
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments