AMKA NA BWANA LEO 21/12/2021
TAA ZINAZOMEMETUKA
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Mathayo 5:16.
▶️ Natamani kuliona kanisa likiamka kwa ufahamu mkamilifu wa jukumu na wajibu wao mbele za Mungu, na kuruhusu nuru yao iangaze ulimwenguni kwa uwazi, imara, na kwa miale angavu. Taa za wengi zinawaka na kufifia, haziwaki vyema na si za uhakika. Zitakuwa kwa wakati fulani zinawaka kwa mwanga mkali na kisha hufifia karibu na kutoweka. Bwana Mungu wa Israeli hawezi kutukuzwa isipokuwa nuru inaangaza vyema katikati ya giza la maadili, sawasawa na kwenye mwanga. Nuru ya Jua la Haki si hafifu. Inaendelea kung'aa juu yetu. Bila kujali ukweli kuwa shetani anatupia kivuli chake cha kuzimu katika njia yetu, nuru inang'aa zaidi ya hapo.
▶️ Je! Ni kwanini sasa wafuasi wa Yesu wasitembee katika nuru Yake, wakiakisi miale angavu ya Jua la Haki? Wanaweza kufanya hivi. Kristo amewaamuru kufanya hivi, na analifanya hili kuwa rahisi kwao kulifanya, kwa kuwa asingewaamuru kufanya kile ambacho sio rahisi kwao kukifanya. Kile kinachowezekana kufanyika na kifanyike, sio tu kwa ajili ya furaha na Amani yao, lakini pia kwa ajili ya uzuri wa dunia.
▶️ Kila siku tunahitaji kuinua roho kuelekea mbinguni, ili ipate miale angavu ya nuru kutoka kwa Jua la Haki. Je! Mungu amesahau kuwapa neema watu wake Wamchao na Wampendao? Hapana. Je! Amezifunga rehema Zake kiasi kwamba haziwezi tena kuwafikia watu wake waliojaribiwa na majaribu? Nawaambieni, haiwezekani. Tazameni juu, enyi roho zitetemekazo na zenye mashaka. Utazameni uso wa Yesu Kristo, wenye kung'aa kwa upendo kwa wale walionunuliwa kwa damu Yake, na msiwe na shaka tena.
🔘 Yesu anaishi kama wakili wenu, Kuhani wenu Mkuu. Yeye ni mwakilishi wenu mbele za Baba katika mahakama ya mbinguni. Upatanisho wake unakuhakikishia kila kitu ambacho Imani yako inakihitaji. "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa" (Mathayo 7:7). Je! Ni nani aliyeyasema haya? Ni Baba wa Milele, na Mfalme wa Amani. Ndiye Mwokozi wako. Kamwe Hatashindwa kuuthibitisha ukweli wa neno Lake. Kamwe hawezi kujidanganya mwenyewe. Mungu ameahidi hivyo. Hebu Imani na idai ahadi.
MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment