BIASHARA UTD WASHTUKIWA KUPOKEA RUSHWA KWA AL AHLI TRIPOLI

Taarifa za ndani kabisa na za kuaminika 100% kutoka kwa Mwanahabari na Mchambuzi Nguli wa Michezo Kutoka nchini Ghana Nuhu Adams, amesema amepokea ujumbe kutoka kwa Rafiki yake wa karibu anaeishi nchini Libya kuwa Klabu ya Biashara United Mara Viongozi wao walipokea Rushwa kutoka kwa Klabu ya Al Ahli Tripoli kiasi ambacho bado hakijajulikana ili timu hiyo ya Biashara isiweze kufika Libya kucheza mechi hiyo ya marudiano.

Nuhu Adams maarufu na ni Mchambuzi, Mwanahabari Nguli kabisa wa Michezo, anafanya kazi katika kituo cha Ghana Soccer, hivyo kwa Habari hii ina ukweli mkubwa ndani yake.

Biashara United hapo mwanzo katika Mechi ya kwanza waliondoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Al Ahli Tripoli katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Katika harakati za kutaka kwenda kukamilisha mechi hiyo ya marudiano ndiyo hali hiyo ikatokea kwa Baishara United kutoonekana Uwanjani nchini Libya na Al Ahli Tripoli kupewa ushindi wa goli 3-0 hivyo Mchezo huo uliisha kwa Aggregate ya 2-3.

Biashara United 2 - 3 Al Ahli Tripoli. AGG.

No comments