WALEZI, WAZAZI WATAKIWA KUJIHAMI NA MATAPELI

"Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa tahadhari kwa wazazi, walezi wa vijana waliomba kuajiriwa na Jeshi la Polisi baada ya kutangaza ajira tarehe 18.08.2021 juu ya matapeli wanaowatumia ujumbe na kuwapigia simu kuwa wanao uwezo wa kuwasaidia kupata ajira hizo"

"Matapeli hao wameanza kuwapigia simu na kuwatumia ujumbe mfupi kuwa wao wapo
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na wengine wapo
katika ofisi za makamanda wa Polisi wa mikoa na kwamba wanaweza kuwasaidia kupitisha majina yao ili wapate ajira"
 
"Watu kama hao ni kama anayetumia namba ya simu 0685 64 31 70 ambaye Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta kwani ameanza kutapeli
wazazi na vijana"

"Jeshi la Polisi nchini linaendelea kuwaelekeza vijana wenye sifa zilizoainishwa katika tangazo la ajira waendelee kufuata maelekezo yanayotolewa na Jeshi la Polisi Makao Makuu kupitia website yake www.polisi.go.tz na maelekezo mengine yanayotolewa na makamanda wa Polisi wa mikoa na pindi mchakato wa kuchambua maombi utakapo kamilika vijana watakaoitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia Polisi Makao makuu na
makamanda wa Polisi wa mikoa na sio kufuata maneno ya utapeli nje ya maelekezo hayo au kutafuta njia za mkato kwani utaishia kutapeliwa"

"Jeshi la Polisi linaendelea kutoa msisitizo kwa wazazi, walezi na vijana waliomba ajira za kujiunga na Jeshi la Polisi wajihadhari na matapeli na pale wanapofuatwa, kupigiwa simu au kutumiwa ujumbe kuwa wanaweza kuwasaidia kupata ajira watoe taarifa katika vituo vya Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa."---- IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi.

No comments