"Serikali imetupatia Fedha Shilingi Milioni Mia tatu, kumi na tano na laki tisa (Tshs 315,900,000) kwa ajili ya upanuzi wa Mradi wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Migongwa kuja Mwamashiga"
"Usanifu umekamilika na ujenzi utaanza ivi karibuni kuweka mtandao wa maji kwa kilometa ishirini na nane kwa ajili ya kunufaisha vitongoji zaidi ya kumi"---- NGASSA
Aidha, Mbunge huyo wa Jimbo la Igunga Mkoani Tabora, Mhe. Nicholaus Ngassa amesema Daraja la Mto Mwamashiga linalounganisha Kata na Kata za Itunduru, Igurubi na Kinungu wanalijenga kwa Fedha za Barabara vijijini wanazopatiwa Majimboni na Serikali.
"----->Mwaka huu tumepata Bilioni Moja na Milioni Mia Tano (Tshs 1,500,000,000), nimewapa nafasi hapa mkutanoni Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) na Mhandisi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) watoe maelezo ya kitaalam kuhusu Miradi hii mikubwa ili Wananchi mpate uelewe na tutembee muelekeo mmoja."---- NGASSA
0 Comments