Advertisement

Responsive Advertisement

RUVU SHOOTING WAJA NA "USIKU WA RUVU SHOOTING"

"Tumeamua kuja na Usiku wa Ruvu Shooting kama ambavyo klabu ya Yanga SC wamefanya ambayo iliitwa "Siku ya Mwananchi" na Simba SC walivyofanya "Siimba Day".

"Sisi Ruvu Shooting tunapita mulemule japo kwa tofauti kidogo, sisi tunasema ni Usiku wa Ruvu Shooting, ambapo itakuwa ni siku ya tarehe 25 mwezi huu"

”Siku hiyo sambamba na kutambulisha wachezaji, pia tutazindua na kutambulisha jezi yetu tutakayoitumia katika msimu huu, kumbuka tuna jezi za aina tatu tofauti, ambazo nina imani hazitakuwa na maswali mara zimebeba nini au zimewekewa nini"

"Pia hatuko nyuma vile vile kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii Aslay Isihaka, Prince Dully Sykes, Tunda Man, Nikk Mbishi pamoja na Dullah Makabila."---- Afisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire.

Post a Comment

0 Comments