Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS WA ZAMANI WA ALGERIA AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 84

Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amefariki dunua akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bouteflika aliongoza nchi hiyo kwa karibu miongo miwili na kuachia madaraka mwaka 2019 baada ya jaribio lake la kugombea muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.

Alikuwa kiungo muhimu katika vita vya kupigania uhuru wa Algeria miaka ya 1950 na 60.

Mwaka 1999, baada ya Algeria kujikwamua kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya karibu watu 200,000, alikuwa raia baada ya kuombwa na jeshi la nchi hiyo.

Bouteflika hajaonekana hadharani tangu mwaka 2013, baada ya kuugua kiharusi ambacho kiliathiri uwezo wake wa kuzungumza na kutembea.

SAFARI YA KISIASA YA BOUTEFLIKA

Kazi yake ya kisiasa ilianza mapema: Baada ya uhuru wa Algeria kutoka kwa Ufaransa mwaka 1962, alikuwa waziri mdogo zaidi wa mambo ya kigeni duniani, rekodi ambayo haijavunjwa hadi wa leo.

Alishikilia nafasi hiyo kwa miaka 16 na alikua mwanachama mahiri wa Umoja wa mataifa.

Akiwa rais wa bunge Umoja wa Mataifa mwaka 1974, alimualika kiongozi wa Palestina wakati huo Yasser Arafat kuhutubia taasisi hiyo ya uongozi ya Umoja wa Mataifa katika hatua ambayo haikutarajiwa na iliyotoa mwelekeo katika siasa za mashariki ya kati.

Pia alisisitiza kuwa China inastahili kuwa na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa, na kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Anasifika kwa kumpatia Nelson Mandela aliyekuwa kijana mdogo mafunzo yake ya kwanza ya kijeshi.

Bouteflika aliishi uhamishoni sehemu ya miaka ya 1980, kuepuka mashtaka ya ufisadi ambayo mweshowe yalifutwa.

Alirejea nyumbani miaka ya 1990 na kuchukua hatamu ya uongozi mwaka 1999 - kama kiongozi wa kwanza wa kiraia wa Algeria ndani ya zaidi ya miongo mitatu.

Mtu huyo aliyejulikana kama "Boutef" alifanikiwa kuongoza mchakato wa amani kati ya jeshi na wanamgambo waliojihami ambao walikuwa wakipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mwaka 2008, alianzisha mchakato wa kubadilisha katiba ya Algeria ambao uliondoa ukomo wa muhula miwili wa marais- na kuchaguliwa tena mara mbili licha ya kukabiliwa na mashtaka ya udanganyifu.

Wakati maandamano ya kupigania mageuzi ya uongozi katika nchi za kiarabu yalipozuka mwaka 2011 kaskazini mwa Afrika, Bouteflika aliongeza haraka ruzuku ya umma na kumaliza hali ya hatari nchini Algeria iliyodumu kwa muda mrefu.

Mara ya mwisho alionekana hadharani ilikuwa mwaka 2017, miaka minne baada ya kupata kiharusi, wakati alipozindua kituo cha metro na msikiti mpya wa Ketchaoua uliokarabatiwa huko Algiers.

Ni katika hafla hiyo ambapo ilitangazwa kwamba rais huyo aliyekuwa akiugua atagombea muhula wa tano mwaka 2019, maandamano yalizuka kupinga hatua hiyo.

Maandamano hayo yalisambaa kote nchini na yalifanyika kila wiki, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tena.

Baada ya awali kuapa kuahirisha uchaguzi na kuondoka madarakani ndani ya mwaka mmoja, Bouteflika alilazimishwa kujiuzulu

Hiyo ndio mara ya mwisho Waalgeria walimuona mtu huyo aliyewaongoza kwa miaka 20.

Post a Comment

0 Comments