MO DEWJI AJIUZULU UENYEKITI SIMBA SC, AMTEUA TRY AGAI
Mwekezaji na Mkurugenzi Mkuu wa Mo Foundation Mohamed Dewji ‘Mo’ ametangaza kuachia ngazi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC na nafasi hiyo amemteua Abdallah Try Again kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.
Mo ametoa tangazo hilo akiweka wazi kuwa sababu kubwa ni ubize wa kusafiri mara kwa mara, na maamuzi hayo waliyachukua baada ya kikao na bodi kilichofanyika Septemba 21, 2021.
Pamoja na kujiondoa kwake atabaki kuwa mwekezaji wa klabu hiyo.
Salim Abdallah Muhene anaefahamika kwa umaarufu 'Try Again' (PICHANI) aliwahi kuwa Mwenyekiti (Rais) wa Simba SC baada ya sakata la Evans Aveva na amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika kipindi cha miaka 4 ya Uenyekiti wa Mohammed Dewji.
Karibu U-Subscribe Youtube Channel Ya Binago
TV Uwe Wa Kwanza Kupata UPDATES Zote, Kwa Kubonyeza Alama Ya Kengele 🔔.
Post a Comment