Advertisement

Responsive Advertisement

MARIO BALOTELI KARUDI TENA KWENYE SOKA KIBABE

Mario Balotelli anayecheza klabu ya Adana Demirspor ya Uturuki, amegonga vichwa vya habari baada ya kumpiga kijembe cha kisasi kocha wa Besiktas.

Ilikuwa katika mchezo wa ligi kuu na timu yake ikiwa nyuma 3-1, Balotelli akafunga 'bonge moja la bao' lililoirudisha timu yake mchezoni.

Katika kushangilia, akakimbilia kwenye benchi la ufundi la Besiktas na kumuonesha kocha wa timu hiyo, Sergen Yalcin, ishara ya kutokuwa na akili kichwani.

Mwaka 2013 Balotelli alipokuwa Manchester City, timu yake ilicheza na LA Galaxy ya Marekani kwenye mechi za maandalizi ya msimu mpya.

Katika mchezo huo, Balotelli alipata nafasi ya kufunga lakini akataka kutia mbwembwe kwa kufunga kwa mtindo wa Al Zidane, lakini akakosa.

Kocha wa timu yake, Roberto Mancini, akamtoa hapo hapo na kumuingiza James Milner.

Wakati huo Sergen Yalcin alikuwa mchambuzi kwenye kituo kimoja cha luninga nchini Uturuki.

Katika uchambuzi wake, akasema Balotelli hana akili hata moja kichwani mwake na yeye ndo angekuwa kocha wake basi angemfukuza kwenye timu.

Ni maneno haya ndiyo yaliyomkera Balotelli na kuyahifadhi moyoni kwa miaka 8 hadi hapo jana sasa alipopata nafasi ya kukutana na kocha huyo.

Mechi ikaisha kwa sare ya 3-3!

Post a Comment

0 Comments