*KESHA LA ASUBUHI.*
*Ijumaa, 24/09/2021.*
*WASHIRIKA NA MUNGU.*
*"Hivyo , apandaye si kitu, wala yeye atiaye maji;bali Mungu akuzaye." 1 wakorintho 3:7.*
▶️ Tunapaswa kuelewa kwamba kama mtu mmoja mmoja tuko katika ushirikiano na Mungu. “ Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka,” Anatushauri, na kuongeza, “ kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema"
( Wafilipi 2:12, 13). Hapa kuna ushirikiano wa Uungu na mawakala wa kibinadamu ...
▶️ Mvua za vuli na za Masika zote zinahitajika. “ Tuwafanya kazi pamoja na Mungu"
( 1 wakorintho 3:9). Bwana peke yake ndiye anayeweza kutoa mvua zenye thamani sana za vuli na za masika. Mawingu, mwangaza wa jua, umande wa siku — Hizi ni riziki za thamani kabisa za mbingu. lakini fadhila zote hizi zitolewazo na mbingu kwa ukarimu zitathibitika kuwa ni za thamani ndogo kwa wale ambao kwa upande wao hawazitengi kwa ajili ya utendaji wa bidii. Jitihada binafsi ni lazima ziwekwe katika kilimo. Kuna kulima na kurudia kulima. Vifaa lazima viletwe na usitadi wa kibinadamu lazima uvitumie. Mbegu lazima ipandwe kwa msimu wake. Sheria zinazotalawa wakati wa kupanda na wakati wa mavumo lazima zizingatiwe, vinginevyo hakutakuwa na mavuno....
▶️ Mtume analeta kielelezo kingine: “ Ninyi ni jengo la Mungu ” ( aya ya 9)- jengo linalopaswa kujengwa. Ujenzi wa jengo unahitaji ustadi wa kutumia mbao ambazo Mungu amesababisha zikue kwa ajili ya furaha na baraka kwa mwanadamu. Bwana ametoa miti ya msituni, na sasa mwanadamu lazima atumie miti hiyo. Lazima ikatwe na kuandaliwa kwa msumeno, na shoka, na kabari, na nyundo, ili ifae kwa ajili ya jengo hilo...
▶️ Hivyo huwasilishwa ushirika wa ubinadamu na Uungu. Uweza wote ni wa Mungu. “ pasipo mimi," anasema kristo, “ninyi hamwezi kufanya neno lolote "
(Yohana 15:5). Basi ni kwa saa ngapi inakuwa salama kwetu kujaribu kufanya kazi pekee yetu? Utukufu wote unatoka kwa Mungu na unapaswa kutirirka kurudi kwa Mungu kwa njia zote zinazowekana, kupitia ushirikiano wetu na Mungu...
▶️ *Tunatakiwa kuzingatia kwa uangalifu masilahi yetu sisi wenyewe ya kiroho. Ikiwa tunakaa ndani ya kristo, hatutakubali shughuli za biashara zenye tamaa ya kutaka makuu, hata katika huduma yetu kwake, kuja kabla ya harufu nzuri ya kiroho ambayo inapaswa kuainisha ushirika wetu na ndugu zetu.*
Usomaji wa Biblia: 1 Wakorintho 16.
Wote tunatamani majibu ya haraka na ya moja kwa moja ya maombi yetu, na tunajaribiwa kukatishwa tamaa majibu yanapochelewa au yanapokuja kwa namna tusivyoyatarajia. Lakini Mungu ni mwenye hekima sana na mwema kuyajibu maombi yetu kwa wakati hasa na namna tunayotamani.
Atatutendea zaidi na kwa ubora kuliko kukamilisha matakwa yetu yote. Na kwa kuwa tunaweza kuzitumainia hekima na upendo wake, hatupaswi kumwomba ayakubali mapenzi yetu, bali tunapaswa kutafuta kuingia na kukamilisha kusudi lake. Matakwa na matamanio yetu yanapaswa kusalimishwa katika mapenzi yake.”—Ellen G. White, Gospel Workers, uk. 219.
“Ilikuwa ni kitambo tu kabla ya Yesu kuja kuwaokoa watoto wake na kuwapatia utimilifu wa kutokufa… Makaburi yatafunguliwa, na waliokufa watatoka wakiwa washindi, wakisema kwa sauti kuu, ‘U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Ewe kaburi, Ku wapi, kushinda kwako?’ Wapendwa wetu wanaolala katika Yesu watatoka wakiwa wamevikwa kutokufa.”*—Ellen G. White, Counsels on Stewardship, 350. *
Masawali ya Kujadili
1. Fikiria kuhusu uhalisia wa pambano kuu. Unalionaje linavyoendelea ulimwenguni? Vipi kuhusu maisha yako wewe binafsi? Je, ni halisi kabisa, au sivyo? Kwa hakika ni halisi zaidi kuliko watu wengi wanavyodhani, kwa sababu watu hawaamini katika uwepo wa shetani halisi. Kwa nini kuelewa uhalisia wa pambano kuu ni muhimu sana katika kutusaidia kuelewa hali ya ulimwengu wetu? Pia, kwa nini uelewa wetu wa jinsi hili pambano kuu litakavyoisha unafariji sana?
2. Unabii unaweza kutukengeusha fikra ikiwa tunajaribu kwenda zaidi ya kile kilichofunuliwa kwa wazi. Ni kwa vipi mara nyingi washiriki wa kanisa wameingia katika matatizo, wakifanya utabiri kuhusu matukio ambayo hatimaye hayakutokea? Tunawezaje kujilinda ili kutoanguka katika mtego wa namna hiyo?
3. Katika darasa, pitia Ufunuo 14:9—11 na swali kuhusu wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake kutokuwa na raha. Hilo linaweza kuwa linamaanisha nini? Mada inayoweza kuleta mabishano katika kanisa ni inayohusiana na wajibu tunaoufanya au tusioufanya katika mpangilio wa muda wa kurudi kwa Kristo. Haidhuru mtu anakuwa na msimamo gani kuhusu jambo hili, kwa nini bado ni muhimu sana kwamba tushiriki katika kusambaza ujumbe wa marejeo yake katika ulimwengu huu?
TAFAKARI NJEMA
0 Comments