Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 23/09/2021

KESHA LA ASUBUHI - Kiswahili & English 

*KESHA LA ASUBUHI* 

 *Alhamisi, Septemba 23, 2021* 

 *YUKO NAMI DAIMA* 

" _Kama nisingelitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na baba yangu"._ Yohana 15:24

▶️ Miujiza yote ya Kristo ilifanyika ili kuwabariki wale ambao wakuu hawa wa Wayahudi waliwapuuza na kuwadharau, na kukataa kuwasaidia. Na Alipendwa sana na watu wa kawaida kwa sababu yeye alikuwa Mponyaji, Mganga Mkuu. Neema zake zote zilikuwa nuru kutoka mbinguni. Katika kila kazi njema Alitafuta kuwaongoza wapate kumpokea kama Mwokozi wao binafsi. Maisha yake yalikuwa ni yenye harufu nzuri, harufu ya uzima iletayo uzima. Alileta uchangamfu moyoni na nyumbani. Walimwendea wakiomboleza, na kuondoka wakiwa na nyimbo za sifa na shangwe na kufurahi. Alijitoa kwao ili wapate kumpa maskani mioyoni mwao.

▶️ Na bado wao (Viongozi wa Kiyahudi) hawakumpokea. Huku wakidai kuishika sheria, Waliikana kwa kazi zao. Huku wakiwa na macho hawakuona, kwa sababu ya ujinga uliokuwa  ndani yao kupitia ugumu wa mioyo yao. Uchafu wa mioyo yao, mazoea yatiayo unajisi ya maisha yao, Ubinafai wao, husuda yao, wivu wao, nia zao mbaya, uvunjanji wao wa sheria ya Mungu, wakati walidai kuishika, ilibeba ushahidi wa daima  juu ya tabia zao halisi. Alitamka kwamba walikuwa wakifundisha mafundisho  yaliyo maagizo ya wanadamu" (Marko 7:7). Tena anasema, "Hamyajui maandiko, wala uweza wa Mungu" (sura 12:24).

▶️ "Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu" (Mathayo 5:8). Wangewezaje kumwona Mungu?— jinsi ambavyo  Henoko alimwona. Walikuwa na fursa ya kutembea na kuzungumza na Mungu. Kwa Imani Henoko aliishi mbele ya uwapo wa Mungu kwa miaka mia tatu. Kwa imani aliiona imani ya Yesu. Alipewa upendeleo maalumu na Yeye. Makuhani na watawala walihitaji uzoefu kama huo aliokuwa nao Henoko. Walihitaji hisi ya daima ya Uwapo wa Mungu. 

▶️ *Ni utajiri mwingi kiasi gani wa neema Bwana alitamani sana kuwapa watu hawa wa Mungu waliopendelewa. Imewakilishwa katika wito wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili yao "Na vyote vimekuwa tayari: njooni" (sura 22:4)*

*MORNING DEVOTION*

Thursday, September 23, 2021

*HE IS ALWAYS WITH ME*

_If I had not done among them the works which none other man did, they had not had sin: but now have they both seen and hated both me and my Father._ John 15:24.

▶️ All Christ's miracles were wrought to bless those whom these leading Jews neglected and despised, and refused to help. And He was beloved [by the common people] because He was the Restorer, the Great Physician. All His graces were light from heaven. In every good work He sought to lead them to accept Him as their personal Saviour. His life was fragrant, a savor of life unto life. He brought sunshine into the heart and home. They came to Him mourning, and left Him with songs of praise and glad rejoicing. He offered Himself to them that they might give Him a home in their hearts.

▶️ And yet they [the Jewish leaders] would not receive Him. While they claimed to keep the law, they denied it by their works. Having eyes they saw not, because of the ignorance that was in them through the hardness of their hearts. The impurity of their hearts, the defiling practices of their lives, their selfishness, their envy, their jealousy, their evil surmising, their transgression of the law of God, while they claimed to keep it, bore continual testimony as to their character. By the fruit the tree was known. Christ laid bare their true character. He declared that they were “teaching for doctrines the commandments of men” (Mark 7:7). Again He says, “Ye know not the scriptures, neither the power of God” (chap. 12:24).

🔘 *“Blessed are the pure in heart: for they shall see God” (Matthew 5:8). How would they see God?—in the way that Enoch saw Him. They had the privilege of walking and talking with God. By faith Enoch lived in the presence of God three hundred years. By faith he saw the faith of Jesus. He was taken into special favor with Him. The priests and rulers needed just such an experience as Enoch had. They needed a continual sense of the presence of God. O what riches of grace the Lord longed to bestow upon the favored people of God. It is represented in the call to the supper prepared for them, “All things are ready: come” (chap. 22:4).*

*GOD BLESS YOU/MUNGU AKUBARIKI *

Post a Comment

0 Comments