Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 22/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI.*

 *Jumatano, 22/09/2021.*

 *JE UMEPITA TOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI?* 

*"Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia  uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiye penda,akaa katika mauti. 1Yohana 3:14.*

▶️ Nimekuwa nikifikiri ni  kidogo kiasi gani tunathamini tamko thabiti la Neno la Mungu kwetu kuhusu Uhusiano wetu kila mtu na mwenzake.
Kuna ubinafsi ule ndani ya moyo wa mwanadamu ambao hulengesha mawazo yetu juu yetu sisi wenyewe; na hata [ndani ya] wale ambao wanaonekana kuwa na uhusiano na Mungu, tunatiwa uchungu wakati mwingine kuona ni kiasi gani cha mawazo yao yamelenga juu yao wao wenyewe, wasione wala kuhisi mahitani ya wengine. 

▶️ Tumeunganishwa pamoja kama vile katika mfumo mkubwa wa ubinadamu, na katika ushirikiano wetu wote tunapaswa kutafuta kwa bidii kuwa na akili ya Kristo. Kuwafumbia macho wahitaji na wanaoangamia, kuwaacha wenye dhambi bila kuonywa na kwa kutojali na ubinafsi kuwajaribu wapate kusema, "Hakuna mtu anayeijali roho yangu". Ni kumfedhehesha Mungu na kuleta shutuma juu ya kusudi la Mungu. Kazi yetu ni kujengana katika imani takatifu kabisa.

▶️ Ikiwa hakuna maelewano kamili kati yetu, hatupaswi kuhisi kwamba sisi wenyewe  hatupaswi  kabisa kulaumiwa katika jambo hilo. Ikiwa mawazo na hisia za mtu mwingine haziko katika njia sawa na yetu, hatupaswi kuhisi kuwa watu wote wamekosea nasi tuko sawa.Tunatakiwa kila wakati  kuweka akili mahali sahihi, ili kujibu ombila Kristo katika Yohana 17:21-23. Tunatakiwa kujua ni nira ipi Kristo anatuagiza kuichukua na mizigo tunayopaswa kuibeba kwa wakati huu,na kujitahidi kila wakati kwa huruma   na Upendo kumwonesha ndugu yetu kwamba  tunavutiwa naye, na kuleta upendo katika matendo yetu siku hadi siku.Hii ndiyo dhahabu iliyojaribiwa katika moto - imani na upendo.

▶️ Ikiwa tutamwona mtu mmoja aliye katika  makosa juu ya jambo lolote hatupaswi kupita bila kusema chochote,  bali ni lazima tujaribu kumtoa  kutoka gizani  hadi kwenye nuru.  Lazima tulinde masilahi ya kila mmoja kama tunavyofanya kwa yetu sisi wenyewe.
Hatuithamini roho kama vile tunavyopaswa. 

▶️ *Inabidi kuungana katika undugu mmoja mkubwa na kuwa mahali pale ambapo tunaweza kusitahimili makosa ya kila mmoja kwa uvumilivu wote na upole, na kujitahidi kubeba  mizigo ya kila mtu na mwenzake ( Tazama Waefeso 5:1,2 .)*
 
▶️ *Sawa, unasema hii ni kazi ya mchungaji. Lakini pia ni kazi ya kila mmoja wetu.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

Post a Comment

0 Comments