AMKA NA BWANA LEO 09/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

Alhamisi, Septemba 09, 2021

*UTAMBUZI WA DHAMBI ZILIZOSAMEHEWA*

*Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.* Yohana 3:30

📖 Ninajisikia huzuni sana ninapoona kukosekana kwa dini ya matendo katikati yetu hasa. Nafsi imeoneshwa zaidi na roho ya Kristo haitambuliwi. Tunahitaji elimu ya kiungu. Tunahitaji kila siku kufanya upya kujitoa kwetu kwa Mungu. 
 
📖 Kwa nini hatuna utambuzi wa dhambi zilizosamehewa? Ni kwa sababu hatuamini. Hatufanyii kazi mafundisho ya Kristo na kuleta manufaa yake maishani mwetu. Kama furaha na kuinuliwa na matumaini yanayogawiwa na Bwana Yesu Kristo yangetolewa kwa wengi wetu, yangeweza tu kutoa kujitukuza na kiburi. Yesu anapokaa moyoni kwa imani, masomo ambayo Kristo ametupa yatatendewa kazi. Tutamwona Yesu Kristo akiwa ameinuliwa kiasi kwamba nafsi itadhiliwa. Upendo wetu utajikita kwa Yesu, mawazo yetu yatavutwa sana kuelekea mbinguni. Kristo ataongezeka, mimi nitapungua. 
 
📖 Akili lazima ifundishwe kufikiri sana juu ya mambo ya mbinguni. Unyenyekevu utakuja kama matokeo ya kutambua uzuri wa Yesu Kristo. Kwa kufikiri sana juu ya ubora wa tabia ya Kristo, tutaona sifa bainifu mbaya ya dhambi na kwa imani tutaielewa haki ya Yesu Kristo. Tutajenga maadili yaliyo ndani ya Yesu, ili tuweze kuakisi kwa wengine mfano wa tabia yake. Tunapoutazama msalaba wa Kalvari, hatutaiinua nafsi, bali daima tutaona kutokustahili kwetu na jinsi wokovu wetu ulivyoigharimu Mbingu; tutautambua upendo wa Kristo usio na kifani.
 
🔘 *Wengi huruhusu akili zao kufikiri sana juu ya kutokustahili kwao kana kwamba huu ulikuwa ni wema. Ni kizuizi kwa kuja kwao kwa Yesu kwa uhakika kamili wa imani. Wanapaswa kuhisi kutokustahili kwao, na kwa sababu ya hii –kwa sababu ya dhambi yao- wanapaswa kuhisi hitaji la kuja kwa Mwokozi, ambaye ndiye stahili yao na ambaye atakuwa haki yao ikiwa watatubu na kujinyenyekeza. Kutokustahili kwao ni ukweli unaojidhihirisha. Kustahili kwa Yesu Kristo ni jambo la hakika. Basi hebu kila roho yenye mashaka iwe na tumaini na ujasiri, kwa sababu ana Yule anayestahili kuwa Mwokozi wake. Tumaini lake pekee la wokovu ni kushikilia kwa imani kule kustahili ambako hana lakini ambako kutatolewa na Yesu Kristo aliye haki yetu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments