Advertisement

Responsive Advertisement

TABIA TULIZONAZO WAKRISTO LEO MAKANISANI

TABIA 10 MBAYA ZILIZOZOELEKA MAKANISANI, AMBAZO NI MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU.

⏺️ Je kati ya tabia hizi, wewe una ipi hapa ili upate kutubu leo???

1. Kuchati au kubofya bofya simu wakati Ibada ikiendelea.

➖ Hii inaonyesha kwamba, unajali sana simu kuliko kile kinachoendelea Kanisani.

2. Kukataa kuketi mahali ambako umeelekezwa na Wahudumu (Kamati ya Ibada) sehemu sahihi ya kukaa.

➖ Hii inaonyesha kwamba, ni jinsi gani ulivyomkaidi na hufuati utaratibu.

3. Upo Kanisani wakati Ibada ikiendelea, ghalfa simu yako inaita kwa sauti ya juu, unatoka nje haraka kwenda kuipokea.

➖ Hii inaonyesha kwamba, huna utii kabisa kwa Muumba wako.

4. Kuchelewa kuingia Ibadani kila siku kwa makusudi.

➖ Hii inaonyesha kwamba, Mungu sio kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako.

5. Kusinzia, kunong'onezana au kupiga story za chini kwa chini wakati wa Ibada ikiendelea.

➖ Hii inaonyesha kwamba, wewe una dharau na hutaki kusikia Neno la Mungu.

6. Kukaa chini muda wote bila sababu za msingi, huku wenzako wakiwa wamesimama au kupiga magoti.

 ➖ Hii inaonyesha kwamba, wewe ni Mjuaji sana na huna maadili kwa Waongoza Sala.

7. Kuangalia saa ya ukutani au ya mkononi kila wakati huku mahubiri yakiwa yanaendelea, kama njia ya kujua leo mahubiri yamechukua muda gani kuisha

➖ Hii inaonyesha kwamba, Neno la Mungu sio sehemu ya maisha yako na huna muda wa kuisoma wala kuitafakari.

8. Kutoshiriki kikamilifu kwenye huduma mbalimbali zinazofanyika Kanisani. Mfano wenzako wanaimba, wewe unatazama huku na kule kuangalia nani aliyependeza leo Kanisani.

➖ Hii inaonyesha kwamba, hukuja Kanisani kwa lengo la kusali, bali kwa lengo la kujionyesha tu ili watu wajue kuwa wewe ni nani.

9. Kuondoka mapema Ibadani kabla haijaisha.

➖ Hii inaonyesha kwamba, unajali sana mambo yako kuliko ya Mungu.

10. Kukusanyika nje ya Kanisa huku Ibada ikiendelea.

➖ Hii inaonyesha kwamba, wale walioko Kanisani ni wajinga sana kuliko wewe uliyeko nje.

⏺️ BASI KAMA UNA TABIA MOJAWAPO KATIKA YA HIZI, NAOMBA UBADILIKE SASA. MAANA MUNGU HUWAPIGA WENYE KIBURI, NA KUWAPA NEEMA WANYENYEKEVU. (1PETRO 5:5-6)

... Mungu akubariki🙌🙌 sana unapo SHARE hii na groups zinginezo. Acha tuweke nidhamu katika nyumba ya Mungu - Yesu yuaja upesi...

Post a Comment

0 Comments