Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 14

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumamosi, 14/08/2021.

*WAKATI WA NUHU NA WETU.*

*Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. Waebrania 11:7.*

▶️Ilikuwa ni kupitia imani na kazi thabiti za Nuhu kwa pamoja ambako kulihukumu ulimwengu. Hakuhubiri tu ukweli wa leo uliofaa kwa wakati ule, lakini alitenda sawasawa na kila hubiri. Kama asingewahi kuinua sauti yake kwa kuonya, matendo yake, tabia yake takatifu kati ya mafisadi na wasiomcha Mungu vingelikuwa ni mahubiri yanye kuhukumu kwa wasioamini na waovu wa wakati huo. Alikwenda kwa uvumilivu na upole kama wa Kristo chini ya matusi, dhihaka, na mizaha. Sauti yake ilisikika mara kwa mara kwa maombi kwa Mungu kwa ajili ya nguvu na msaada Wake ili apate kutenda amri zote za Mungu. Hii ilikuwa ni nguvu iliyo wahukumu wasioamini.

▶️Lakini wakati unakuja ambapo wito wa mwisho wa Nuhu unafanywa kwa jamii yenye hatia. Anawambia kwa mara nyingine tena wapate kuutii ujumbe wa onyo na kupata kimbilio ndani ya safina. Ananyosha mikono yake kwa dua na sauti iliyojaa huruma. Kwa mdomo unaotetemeka na macho yaliyojaa machozi, anawaambia kazi yake imekwisha, lakini kwa sauti kubwa, dhihaka na kejeli na matusi yasiyo na adabu yaliyo dhahiri zaidi yanalundikwa juu ya Nuhu. Mwenye ari, mshupavu wa kidini, kichaa, huanguka kwenye sikio lake. Anawaaga wote, yeye na familia yake wanaingia ndani ya safina, na Mungu anafunga mlango. Mlango ule uliomfungia Nuhu ndani, uliufungia ulimwengu nje. Ulikuwa ni mlango uliofungwa katika wakati wa Nuhu. Na Bwana alimfungia ndani. Hadi kufikia wakati ule, Mungu alikuwa amefungua mlango ambao kupitia huo wakazi wa ulimwengu wa zamani wangeweza kupata kimbilio ikiwa wangeliamini ujumbe uliotumwa kwao kutoka kwa Mungu. Lakini mlango huo sasa ulikuwa umefungwa na hakuna mtu aliyeweza kuufungua. Muda wa majaribio ulimalizika.

▶️Uvumilivu wa Mungu wa muda mrefu ulikuwa umekoma, takwimu katika vitabu vya Mungu vya hesabu zilikuwa zikiongezeka, kikombe cha wasio haki kilijaa. Rehema ilikoma na ndipo haki ikachukua upanga wa kulipiza kisasi....

▶️ *Kulikuwa na mlango uliofungwa wakati wa Nuhu. Kulikuwa na mlango uliofungwa kwa wasioamini katika maangamizo ya Sodoma, lakini mlango uliofunguliwa kwa Lutu. Kulikuwa na mlango uliofungwa kwa wenyeji wa Tiro, mlango uliofungwa kwa wakazi wa Yerusalemu... Ambao hawakuamini, lakini mlango wazi kwa wanyenyekevu, wanaoamini, wale waliomtii Mungu. Ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

Post a Comment

0 Comments