TOKA GHARIKA HADI KIFO CHAKE YESU MSALABANI

*TOKA GHARIKA HADI KIFO CHAKE YESU MSALABANI*
Unabii wa karne na karne
Katika somo lililopita tuliona watu walioishi miaka 2000 ya kwanza waliangamizwa kwa gharika zama za Nuhu, na dunia ikaanza upya ikiwa na watu wanane. 1Petro 3:20.

MUNGU huwa haangalii wingi wa watu, bali huangalia ni nani aliye mwaminifu kwake anayemtii na kuziishi sheria zake na maagizo yake.

Wakati gharika iliposhuka kwa nguvu kubwa, shetani alihofia maisha yake, alikuwa hajawahi kuamini kama MUNGU anaweza kuangamiza viumbe vyote, Shetani aliogopa.

Leo tutaangazia tena miaka 2000 ya pili na maisha yalivyoanza, na kilichotokea katika hiyo miaka toka gharika hadi kifo cha KRISTO msalabani.

Turejee unabii wa KRISTO kwa adamu👇🏻👇🏻

👉🏻👉🏻  Hivyo kwa adamu yalifunuliwa matukio muhimu katika historia ya mwanadamu, kutoka ambapo kauli ya Mungu ilitangazwa edeni hata katika gharika, na kuendelea hata ujio wa kwanza wa YESU . Alionyeshwa kwamba wakati kafara ya KRISTO ingekuwa yenye thamani ya kutosha kuokoa ulimwengu mzima , wengi wangechagua maisha ya dhambi kuliko toba na utii.
#Patriarchs &Prophets . P, 67.3

Baada ya gharika tukio lililokuwa limetabiriwa ni ujio wa kwanza wa Yesu.

Je kwanini MUNGU asingewakomboa nuhu na familia yake tu na kuwapeleka Mbinguni ??

#Kusudi la pambano kuu ni kufunua kuwa ni nani kati ya kristo na shetani anapaswa kuabudiwa, hivyo kufunuliwa kwa kristo kama mkombozi wetu na mfalme hakukutimia katika miaka ile ya 2000 ya kabla ya gharika, maana yeye aliye dhabihu ya kweli alikuwa hajaja bado.

#Mwanzo 3:15👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Uzao wa mwanamke utamponda kichwa shetani, na shetani atauponda kisigino uzao wa mwanamke.

👆🏻👆🏻👆🏻 hayo mambo mawili hayakutimia katika gharika.

TUONE MAANA YA HAYO MANENO MAWILI.

Wimbo ulio bora 5:1-7👇🏻👇🏻👇🏻

Sulemani anaeleza tukio ambalo anavuviwa na Roho wa Mungu.

#Aliingia bustanini achume manemane na rihani, akiwa anakula sega la asali na divai na maziwa, anawaagiza na marafiki zake wakale, wanywe, wapendwa wake.

#Ghafla alipokuwa amelala , lakini moyo wake ukiwa macho akasikia sauti ya mpenzi wake, hua wake, mkamilifu wake, na kichwa chake kimelowa manemane na nywele zake manyunyu ya usiku.

#Akiwa amevua kanzu yake , anahangaika aivaeje, na pia akiwa anaogopa asiichafue, ila sauti ya mpenzi wake imemchoma.

#Akaondoka amfungulie, lakini kitu cha kuumiza alipofungua akakuta mpenzi wake kageuka, keshaondoka. Alizimia nafsi yake kwa uchungu aliponena, akamtafuta asimpate, akamwita asimwitikie.

👉🏻👉🏻👉🏻👉🏻 Hili tukio ndilo lililotokea edeni kati ya Kristo na kanisa lake(adamu na mkewe)

#Bwana alikuwa anakuja mara kwa mara kwa Adamu na mkewe bustanini, lakini siku moja alikuja bustanini kisha akachuma vitu vilivyompendeza na akawaambia marafiki zake wafurahie pamoja naye na kula(hawa ni malaika waliokuwa wakija edeni kila wakati) kisha alirudi mbinguni. Sulemani alivuviwa kuwa akalala ila moyo wake ukiwa macho.

#Kanzu aliyokuwa ameivaa ni vazi la utukufu wake. YESU aliogopa kuchafua asili ya uungu wake, wala kuvua utukufu wake. Lakini akiwa MBINGUNI alisikia sauti ya mpenzi wake mkamilifu👉🏻 Kanisa lake likibisha hodi mlangoni ambalo ni kamilifu halijatenda dhambi lakini tayari limegeuka.

#Hii ni pale mke wa adamu alipokula tunda la ujuzi wa mema na mabaya na pia adamu naye akala. Wote wawili walikuwa na ufahamu kama Mungu wa kujuwa mema na mabaya. 👉🏻👉🏻👉🏻👉🏻Jambo hili lilikuwa kama hodi mbinguni, kwamba walitaka kuingia mbinguni.

#Bwana akaondoka awafungulie mlango(Kanisa mpenzi wa KRISTO). Lakini alipofungua hakuona mtu, 👉🏻Kanisa lilijificha.

👉🏻sulemani asema, Lakini mpendwa wangu amegeuka, amepita, akaita asisikie, akamtafuta asionekane.

👉🏻#Mwanzo 3:8-9
Kisha wakasikia sauti ya BWANA MUNGU akitembea bustanini wakati wa jua kupunga, Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani BWANA MUNGU asiwaone. BWANA MUNGU akamwita adamu akamwambia uko wapi??

KRISTO aliumia sana moyoni, mpenzi wake alikuwa amegeuka, ameasi, aliyekuwa mkamilifu , amekuwa mdhambi, KRISTO alizimia nafsini mwake.

Wimbo ulio bora 5:7
Walinzi wazungukao mjini waliniona wakanipiga na kunitia jeraha, walinzi walindao kuta zake wakaninyang'anya shela yangu. 👉🏻👉🏻👉🏻 Soma 👇🏻👇🏻
Mathayo 27:27-31, 34-35

Biblia inasema walinzi wazungukao mjini, siyo bustanini. Walinzi hao wazungukao mjini walimuona wakampiga na kumtia jeraha, wakamnyang'anya shela yake. Alienda mjini kumtafuta mpenzi wake aliyemgeuka akapotea.

👉🏻Kristo alipoteza kanisa lake edeni, alikuja tena duniani kulitafuta kanisa, lakini walinzi wa mjini(binadamu wadhambi) walimuona YESU wakamkamata wakamvua shela yake, wakampiga hata mauti ya msalaba. Lakini KRISTO alifufuka na akabaki na alama za jeraha walizomsababishia hawa walinzi wa mjini.

MAANA YA KUPONDWA KISIGINO NA KUPONDWA KICHWA.

Manuscript Releases vol 18.
        P 72.2-3
Kupitia wale waliomdhihaki KRISTO walipomtundika juu ya msalaba, Shetani na malaika zake waliwakilishwa, aliwajaza na maneno machafu na maovu, aliwavuvia dharau, lakini kwa hayo yote hakufaidika chochote. Aliruhusiwa kuponda kisigino cha KRISTO , Lakini KRISTO alikuwa akiponda kichwa chake. Kwa kutenda kazi kupitia makuhani dhidi ya KRISTO , Shetani alikuwa anazidi kuathuri anguko lake na usumbufu wake mwenyewe.

#kama dhambi hata moja ingeonekana ndani ya KRISTO ulimwengu ungemezwa katika giza na uharibifu.

1MR 11.3
Waliona rehema za MUNGU kwa mifano, ahadi iliyotolewa kwa adamu na eva pale edeni ulikuwa ndiyo injili ya ubinadamu ulioanguka, ahadi ilifanya kuwa uzao wa mwanamke utamponda kichwa shetani, na yeye atamponda kisigino.

KRISTO Yesu kama mkombozi atafunuliwa mara tatu.

1. Kwenye gharika KRISTO YESU alijifunua kama safina. (Miaka 2000 ya kwanza)
2. Msalabani YESU alifunuliwa kama mwanakondoo wa kafara aichukuaye dhambi ya ulimwengu . (Miaka 2000 ya pili)
3. Wakati wa kuja kwake mara ya pili KRISTO atafunuliwa kama Mfalme wa wafalme na BWANA wa mabwana.(miaka 2000 ya tatu).

JE ILIKUWA NI MIAKA MINGAPI HADI KRISTO ANAFUNULIWA MARA YA PILI BAADA YA GHARIKA.??

Danieli 9:27
Katikati ya juma atakomesha kafara na dhabihu.👇🏻👇🏻👇🏻

Katika mwaka wa 31AD, miaka mitatu na nusu baada ya ubatizo wake, BWANA wetu alisulubiwa . Dhabihu kuu iliyotolewa karvari ilikomesha utaratibu wa dhabihu za kuteketezwa ambazo kwa mda wa miaka 4000 zilikuwa zikielekeza kwa mwanakondoo wa Mungu . Mfano ulikuwa umekutana na halisi, na kafara na dhabihu zote na taratibu za kutoa kafara zilikomea pale.
        Great Controversy P. 327.3

KRISTO alikuwa amesimama kwenye hatua ya kuvuka majiji mawili na sikukuu zake kubwa mbili. Yeye mwanakondoo wa MUNGU asiye na waa (dhambi) karibu alikuwa anaelekea kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu ya dhambi, ili kwamba aweze kukomesha mifumo  na sikukuu ambazo kwa miaka 4000 zilielekeza kwenye kifo chake. Desire of ages pg 652.

Shetani alimwangusha mwanadamu katika dhambi, na mpango wa ukombozi uliwekwa tayari kutenda kazi. Kwa miaka 4000 kristo alijishughulisha katika kumwinua mwanadamu . Desire of Ages p 760

Lakini YESU aliupokea ubinadamu wakati ubinadamu umedhohofishwa kwa miaka 4000 ya dhambi. kama ilivyo kwa kila mtoto wa mwanadamu alipokea matokeo ya utendaji kazi ya sheria kuu ya urithi.. Desire of Ages p 49.

👉🏻 Kwa hiyo toka kafara ya kwanza iliyotolewa edeni na kuendelea hadi KRISTO anakufa msalabani ni miaka 4000 kamili ilitimia bila kukosea. Wakati kutoka edeni Adamu alipotenda dhambi siku ile na MUNGU akatangaza Pambano Kuu hadi wakati wa gharika ni miaka 2000, na kutoka gharika hadi YESU anakufa msalabani ni miaka 2000, . Hivyo juma ni miaka 4000.

BWANA alianzisha mfumo wa kutoa dhabihu na adamu baada ya anguko lake, ambao aliwafundisha na uzao wake. Mfumo huu ulichafuliwa baadaye kabla ya gharika, lakini tena ulichafuliwa na wale waliojitenga  wakaenda kujenga mnara wa babeli.
       Story of redemption  P. 149.3

Hivyo baada ya miaka 2000 toka gharika , Yesu anafunuliwa tena kwa njia ya msalaba. Wakati katika gharika alifunuliwa kwa njia ya safina.

Pamoja na YESU kufunuliwa kwa awamu mbili, mbona uovu haukomi??

👉🏻 Ni kwasababu shetani bado yupo hai. Uovu utakoma pale shetani atakapotwishwa dhambi zote kichwani pake kama mbuzi wa azazeli na kuuawa pamoja na malaika zake waovu.

Wanadamu walipoongezeka juu ya duna baada ya gharika walimsahau MUNGU tena. Ulimwengu wote uliharibika, dhambi zilizosababishwa sodoma na gomora kuchomwa , bado zinatendeka. CTBH p 43.2

Ndoa za wake wengi zilikuwa moja ya dhambi zilizosababisha ghadhabu ya MUNGU kabla ya gharika. Lakini baada ya gharika zilienea tena.
From Eternity Past . P 236.2

👉🏻Tafakari upendo wa Mfalme alikuja mjini kumtafuta mpenzi wake , lakini akapigwa akajeruhiwa, akanyang'anywa shela yake na walinzi wazungukao mjini. YESU anatupenda mno ajabu.

Miaka 4000 ilishapita. Biblia inasema . Yeremia 8:20-21
👉🏻 vipindi vyote viwili vimepita, lakini bado hatujaokolewa.
Nafasi iliyobakia ni miaka 2000 ya mwisho.

👉🏻👉🏻👉🏻Miaka 4000 ilikamilika mwaka 31AD katikati ya mwaka wakati YESU alipokufa msalabani. Toka adamu alipoanguka dhambini na kuamriwa kutoa kafara hadi YESU alipokufa msalabani kuwa kafara ya dhambi zetu , ilikamilika miaka 4000

👉🏻Toka edeni hadi gharika ni miaka 2000.
👉🏻Toka gharika hadi kifo cha YESU ni miaka 2000.
👉🏻Jumla ni miaka 4000.

Mjumbe wa MUNGU anasema👇🏻👇🏻👇🏻

Naliona malaika wanne ambao walikuwa na kazi ya kufanya juu ya nchi na walikuwa njiani kuimaliza. YESU akiwa amevikwa mavazi ya kikuhani alitazama kwa huruma juu ya masalia, kisha aliinua mikono yake na kwasauti ya huruma alilia, Damu yangu Baba, damu yangu, damu yangu, damu yangu. Kisha naliona mwangaza mkali kutoka kwa Baba aliyeketi juu ya kiti cha enzi cheupe na ulimulika kumzunguka YESU . Kisha naliona malaika akiruka kwa kasi kwenda kwa wale malaika wanne ambao walikuwa na kazi ya kufanya duniani, na alipunga kitu fulani juu na chini kwenye mkono wake , na alilia kwa sauti ya juu, shikilieni, shikilieni, shikilieni mpaka watumwa wa MUNGU watiwe muhuri katika vipaji vya nyuso zao. Christian Experience and teachings  P 102.1

Mpendwa msomaji, mambo yanakaribia kufika ukingoni. Huko mbinguni katika chumba cha patakatifu Pa patakatifu, Yesu anawatazama Wanadamu kwa huruma sana. Anatamani tumkimbilie atufiche mbawani mwake dhidi ya ghadhabu inayokuja. YESU anaijuwa hasira ya babake pale uvumilivu wake unapokoma kwa Wanadamu wadhambi.

👉🏻Ajabu dunia ya leo Wanadamu wanajipanga kumpinga MUNGU duniani  pamoja na watumwa wake wanaomtii. Mataifa yanajipanga kumkataa MUNGU wa kweli ili yakaabudu kiumbe.

👉🏻Miaka michache ijayo tutashuhudia mambo mabaya katika hii dunia.

Mwisho umekaribia kabisaaa.

Mwisho wa somo la miaka 2000 ya pili.  Toka gharika hadi kifo cha Shujaa mwana wa MUNGU msalabani.

Fatilia miaka 2000 ya tatu na ya mwisho na tunafunga historia ya dunia.

Ni mimi mjoli mwenzako.
Pambano Ibrahim Chindema .

BWANA awabariki

No comments