Advertisement

Responsive Advertisement

SERIKALI KUOKOA BILIONI 33 KWA MWAKA

Serikali itaokoa Bilioni 33 kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa Dawa na Vifaa tiba baada ya kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya dawa na Vifaa tiba kinachojengwa Mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Idofi-Makambako mkoani hapa.

"Hapa nimeangalia takwimu zako Mkurugenzi tunapoenda kukamilisha kiwanda hiki Cha mipira ya mikono(gloves), Dawa za vidonge (tablet), vidonge vya rangi mbili (Capsules) na dawa za maji(Syrup) Serikali kwa mwaka inakwenda kuokoa Bilioni 33 ambazo zingehitajika kununua mahitaji hayo".

Aliongeza kuwa Serikali ingehitaji Bilioni 33 zaidi ili kwenda kununua dawa na Vifaa hivyo sehemu nyingine ndani au nje ya nchi lakini hizo Bilioni zinazoenda kuokolewa tunakua tumeshazalisha kwa gharama za uzalishaji kwa mwaka Bilioni 15.

"Ina maana hii Bilioni 33 inayobaki ukigawanya kwa milioni 700 ambayo ndio gharama za Kujenga vituo vya afya na Vifaa vyake kwa 'force account' Ni sawa na kujenga vituo vya afya 43".Alifafanua Dkt.Gwajima

Alisema Mradi huo unafanya kutimiza azma ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Ilani yake inayosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na uwezekano wa kupunguza gharama za kununua bidhaa ambazo tunaweza kuzitengeneza badala ya kuzinunua nje zitanunuliwa hapa hapa.

"Lengo ni kupunguza gharama za Serikali kutafuta mahitaji ya kuwahudumia wananchi Kwenye eneo la Afya hususani Watoto wachanga,Wajawazito na Wazee.

"Tunapowekeza kiwanda hiki hapa tunatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ,Serikali ya awamu ya sita kujielekeza Kwenye kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali".Alisisitiza

Aidha, amewapongeza MSD kwa kusimamia mradi huo kwa kutoka Kwenye maandishi na kwenda Kwenye uhalisia"Nawapongeza sana Bodi,Uongozi na Wafanyakazi wote wa MSD kwa kusimamia Jambo hili kwani sio Jambo jepesi, na lina Vita vya kutosha,sio watu wote wanapenda ilani itekelezwe.

Post a Comment

0 Comments