Advertisement

Responsive Advertisement

NIKK WA PILI AKAMILISHA MAKTABA YA TEHAMA

Nickson Simon John amesema, Rais Samia Suluhu Hassan, ana nia ya dhati katika kuhakikisha elimu yetu inajikita kwenye kutoa ujuzi. 

"----->Jambo hili limeelekezwa pia kwenye ilani ya CCM, kwamba ujenzi wa uchumi unategemea watu wenye ujuzi na maarifa"

Aidha, amesema katika kutekeleza hayo hapa Kisarawe, wamekamilisha maktaba ya TEHAMA katika shule ya sekondari #JokateMwegelo kupitia mfuko wa #P4R chini ya TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau kama Vodacom Foundation.

"Pia tumetenga bajeti kujenga maktaba za TEHAMA kwenye shule 9 za sekondari kupitia mfuko wa SEQIP"

"----->Mimi nasadiki katika maneno ya ‘Kizaramo’ kwamba “Digital is now and Future”, lazima elimu yetu iwajenge vijana wa nchi hii kuwa na ujuzi, hususan kwenye TEHAMA. Kwa dira hii tunayoelekezwa na Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, tutafika huko." NIKKWAPILI

Post a Comment

0 Comments