RAIS WA UFARANSA AMTUNUKU NISHANI BALOZI RADHIA MSUYA
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemtunukia Balozi Radhia Msuya wa Tanzania, nishani ijulikanayo kama “National Order of Merit”. Balozi Msuya amevikwa nishani hiyo na Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier.
Hafla fupi ya kumtunuku Balozi Msuya nishani hiyo imefanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 17 Aprili, 2021.Balozi Radhia Msuya ametunukiwa nishani hiyo kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Ufaransa wakati akiwa Mkurugenzi wa Ulaya na Marekani.
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (2006-2010). Ametambuliwa kwa mchango mahsusi aliyoutoa wakati Ufaransa ilipokuwa Rais wa Umoja wa Ulaya.
Nishani hiyo ilianzishwa 1963 kwa nia ya kutambua mchango wa watunukiwa ktk kuendeleza ushirikiano na Ufaransa katika ustawi wa dunia.Baadhi ya watu mashuhuri waliotunukiwa nishani ni Rais François Mitterrand wa Ufaransa Mfalme Juan Carlos wa Uhispania na Njoroge Mungai wa Kenya.

Post a Comment