OLE SABAYA NA WENZAKE WASOMEWA MASHITAKA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya (34) nabWalinzi wake watano wamesomewa makosa mbalimbali yakiwemo Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha na kupokea
Rushwa ambayo hayana dhamana.

Wanatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, Uhujumu Uchumi, kujipatia Fedha kwa njia ya Rushwa na Utakatishaji Fedha ambapo Sabaya alijipatia Tsh. Milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara, Francis Mroso, ambaye alituhumiwa kwa ukwepaji kodi.

Pia, walimpiga Bakari Msangi ambaye ni Diwani wa CCM Kata ya Sombetin na kumuibia Tsh. 390,000. Pia, wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Tsh. 35,000.

No comments