NENO KUU MAKAMBINI LEO 28
*SOMO:PAMOJA NA YESU NITAKWENDA ZAIDI YA KAWAIDA.
*Pr. ERASTO NZUMBI.
*TRH 28 JUNE 2021
*MAKAMBI TANGA JIJI
💞Daniel 6:1-2 .....Daniel katika tundu la simba.
✓Mambo muhimu:
1. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa mtu wa faida. Mfalme Dario anachagua watu 3, na moja wapo alikuwa Daniel kuwa msaidizi wa mfalme. Alikuwa mtu mwenye faida kwa sababu ya uchapa kazi wake.
Kuna watu wafaida kama hawa...
*Nelson mandela
*JK Nyerere.
*Bahati Mangazi india
*Mama Tereza
*Martin Luther King
*George Washington.
Hawa ni watu baadhi tu ambao wameacha alama katika mataifa yao. Je ww umeacha alama unapoishi?
2. Kamwe usiruhusi sifa na mambo ya dunia hii yakutenge mbali na Mungu. Sawazisha standadi yako ya ukristo.
✓Daniel mambo yake hayakumtenga na Mungu wake, hata alipokuwa chini na bado alipopandishwa cheo alizidi kuwa mnyenyekevu kwa Mungu
Warumi 8:35-39
✓Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Kama ilivyoandikwa, ya kwamba,
Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa,
Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
✓Usitengwe na upendo wa Kristo. Umebarikiwa kupata mali lkn unalingaaaa...! Maisha yako na vitu vyako ulivyonavyo visikutenge na Mungu wako.
✓Nakutia moyo tunza hadhi yako ya ukristo ktk ya...mila na desturi, kufukuzwa kazi, uchumba, misukumo, ushawishi wa kutoa mimba, rushwa , magonjwa, operation, mali, elimu, interview, uyatima, ujane, ugane, kuteswa, kukosa mtoto, kufirisika..n.k, Tunza hadhi yako ya ukristo kama Daniel.
✓Katika kambi hili kuna watu watamtetea Mungu kila mahali na watasimama imara juu ya utakakatifu wao.
3. Kadri unavyoendelea kufanikiwa ndivyo unavyoongeza maadui.
✓Danieli 6:5-9...
Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.
✓Wivu kwa daniel..hata kwa washiriki wote, mtu kanunua tu gari inakuwa shida, anaimba vizuri shida, kupanda cheo shida, kila kitu shida. Hata kwa Daniel ilikuwa hivyo.
✓Daniel alikuwa mgeni ktk nchi na gafla anapandishwa cheo lkn wenzake wakatafuta njia ya kumharibia ukuu wake lkn alisimama imara, nakutia moyo kuwa imara kama daniel.
✓Daniel alizidisha maombi mara 3.... Danieli 6:10-11.Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
✓Pamoja na Yesu nitakwenda zaidi ya kawaida. 2 Mambo ya Nyakati 7:14-15
...ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.
✓Shetani anaharibiwa pale watu wa Mungu wanapoomba...Muulize samsoni, sarah, Hanna, shadrack meshaki na abedinego, paulo, sirah, watu wa ninawi,... Jizoeze kuwa mtu wa maombi na utafanikiwaaaaa!
✓Mwisho wa yote Daniel anaingizwa kwenye tundu la simba na hakulalamika,acha kulalamika tuliza boli weka mpira centre ucheze mpira....Mungu wetu atakupigania hadi ile dakika ya mwisho. Usikate tamaa wala kulalamika, Malaika wanatua kwa daniel shimoni na kufunga makanywa ya simba na Daniel akawa salama.....!
Mungu Akubariki.
Post a Comment