MUSEVENI AKUBARI KUFANYA MAOMBI KWA NCHI YAKE
Kama Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza Juni 24, 2021 kama nafasi kwa Wananchi kushiriki maombi.
Katika ilani iliyochapishwa Alhamisi, Rais Museveni aliitangaza kama siku ya kitaifa ya sala juu ya janga la Covid-19.
"Nimekubali ombi kutoka kwa viongozi wa kidini kuliweka wakfu taifa kwa maombi wakati wa vita vyetu dhidi ya COVID-19. Natoa wito kwa nyinyi wote kuwaombea wataalam wetu wa afya na kwa familia tofauti ambazo zimeathiriwa. Kwa hivyo, ninatangaza mpaka Ijumaa itakuwa ni nafasi kwa wananchi kushiriki ipasavyo kuiombea nchi yetu "rais wa Uganda alisema.
Taifa hilo la Afrika Mashariki lilikuwa limeripoti visa 74,260 vya Covid-19 kufikia Alhamisi na vifo 752 tangu kesi yake ya kwanza kuripotiwa.
Post a Comment