MAMBO 10 NA ALI KAMWE

Mambo 10 aliyoyaona Mchambuzi ALi Kamwe katika mchezo wa Simba SC dhidi ya Mbeya  City leo, ambapo Simba ameibuka mshindi wa Goli 4 - 1.

1: Another System. Another Great Perfomance Shikamoo 'Master' Didier Da Rosa.. 4G IMESOMA kwenye mnara kuelekea Tar 3

2: Simba walikuja na system ya 3-5-2, Miquissone na Bwalya wakicheza mbele ya Morrison na Bocco. Wapi Simba walifanikiwa kwa dakika 45 za kwanza?

3: Mabeki watatu wa Simba walipunguza madhara ya counter attack za Mbeya. Viungo watano wakatengeneza faida ya watu wengi katikati ya kiwanja. Mtego huu ukawavuta mabeki wa pembeni wa Mbeya kuingia kati na kujikuta wakinasa kwenye mtego mwingine wa kufungua njia za Tshabalala na Kapombe.. SIMBA WAKAUTALAWA MCHEZO

4: Kocha wa Mbeya City ni kama alijaza maelekezo mengi kwenye vichwa vya wachezaji wake. Dakika 45 wakakimbia sana uwanjani bila Target. Haikujulikana wanaanza kukaba kwenye Line ipi. 

5: Kipindi cha Pili, Mbeya City wakarisk kwenda kwenye High Line. Ikawasaidia kuwapress viungo wa Simba na kutumia faida ya makosa yao! BUT hii iliwafanya wawe wazi na Simba kushambulia kwa kasi kwenye eneo lao. Wakanasa tena kwenye mtego

6: NYONI Ni kwa sababu anacheza katika kikosi chenye mastaa wengi ndio maana hatumuimbi sana. Nafikiri faida yake itaonekana siku akitundika daruga! Nyoni ndiye anayempa kiburi Da Rosa kubadili System zake.Kuna kazi kikubwa aliifanya mbele ya viungo wa Mbeya City wasielewe cha kufanya.. WHAT A PLAYER!

7: Kibu Deniss ni kama alikuwa anacheza akiliwaza gazeti la Mwanaspoti kesho! Alipania mno na mwisho wa siku kuna maamuzi akawa anayafanya kwa ajili yake na sio Timu

8: Miquissone! Anacheza kwa moyo wake. Bila shaka mchezo wa soka ni kitu amachokipenda sana! Mahala ambapo ni ngumu mchezaji mwingine kutia mguu, Miki anameza ustaa wake, anakandamiza bila woga.. 

9: Morrison alikuwa vyema kwenye kuanzisha mashambulizi, lakini Mbeya City walipoanza kuwapress viungo wa Chini, huduma kwake ikakata. Ni ngumu kumkaba lakini vijana wa Mbeya wametoa somo zuri jinsi ya kudili na hatari zake. Kata umeme kutokea chini

10: System mpya ya Da Rosa ilikuwa rafiki kwa Tshabalala na Kapombe! What a Perdomance Nilipenda ile pasi ya rambirambi ya Kapombe kwa Chama.

Nb: Huku Chama karudi.. Huku Manji karudi.. Tar 3 PATAMU 😀

UNAMPA BIG YES? OR BIG NOO?

No comments