JINSI BAJETI KUU ILIVYOGUSA MAENEO YA TAMISEMI

1. Fedha za nyongeza Tsh Bil. 322 kujenga barabara za Vijijini kupitia TARURA. (Barabara bora kila kijiji).

2. Fedha za nyongeza Tsh. Bil. 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Maboma ya Zahanati Nchi Nzima 2021 22.

3. Fedha za Nyongeza Tsh. Bil 100 kwa ajili ya ununuzi wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi.

4. Fedha za nyongeza Tsh. Bil. 125 Kukamilisha ujenzi wa maboma ya madarasa 10,000 kwa shule za msingi na Sekondari Nchi nzima.

5. Serikali kuu kulipa moja kwa moja posho za mwezi kwa madiwani katika Halmashauri 168.

6. Posho ya mafuta ya Tsh. 100,000/- kila mwezi kwa Watendaji Kata nchi nzima.

7. Posho ya Mafuta Tsh. 100,000/- kila mwezi kwa Maafisa Tarafa nchi nzima.

No comments