JAFO ASEMA KUTUMIA GESI ASILIA ITAJENGA UCHUMI NCHINI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amelitaka Baraza la Taifa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Samuel Gwamaka kuhakikisha vituo vyote vipya vya mafuta vizingatie uwepo wa sehemu iliyotengwa kwa ajili ya gesi asilia ndipo litoe cheti cha usajili.
Ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa gari linalotumia mfumo wa gesi asilia iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Kampuni ya magari ya Scania na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
“Umefika wakati sasa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upande wa mazingira tunapotoa vyeti vya mazingira kwa ajili ya vituo vya mafuta ni lazima viwe na sehemu maalumu ya kuwekea gesi asilia ili kurahisisha upatikanaji wa gesi itakayotumika kwenye magari yanayotumia gesi hiyo,” alisema Jafo.
Aliongeza endapo Tanzania itatumia gesi asilia kwenye magari itakuwa imepiga hatua kubwa katika utunzaji wa mazingira hasa kwenye eneo la kuzuia uchafuzi wa hewa na uchafuzi wa kelele unaosababishwa na magari yanayotumia mafuta.
Alisema utumiaji wa gesi kwenye magari utasaidia kujenga uchumi imara wa nchi yetu kwasababu gesi itakayotumika ni ya hapa hapa Tanzania, hivyo alilisitiza wawekezaji wajitokeze kwa wingi kuwekeza kwenye gesi asilia ili rasilimali hii itumike na kuleta manufaa kwenye nchi yetu.
“Zaidi ya ujazo trillion 57.54 za gesi zinapatikana Tanzania lakini matumizi yake bado hayajafika ujazo wa trillioni 1, hivyo niwaombe wawekezaji kutumia fursa hii kuwekeza kwenye nishati hii kwasababu ipo ya kutosha na tutaepuka gharama zisizo za lazima kuagiza mafuta nje ya nchi,” alieleza Jafo.
Waziri Kalemani alisema Tanzania inaongoza kwa gesi nyingi kulinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki hivyo ni utajiri mkubwa unaohitaji uwekezaji makini utakaoleta manufaa ya kiuchumi katika nchi yetu. Amesema umeme unaotumika Tanzania ni zaidi ya asilimia 70 unatokana na gesi asilia.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC James Mataragio aliwahakikishia wawekezaji wa gesi kuwa Serikali kupitia TPDC inachukua hatua mbalimbali kwa ajili kuhakikisha gesi inayopatikana inasambazwa maeneo mbalimbali nchini.

Post a Comment