UPENDO AU MSISIMKO

*UPENDO🤝🏽 MSISIMKO* 
Nafahamu kichwa cha somo hupelekea kufikiria utofauti wa upendo halisi💖na msisimko tu🔥. ```Lakini umewahi jiuliza🤔 Kuna mfanano gani Kati ya upendo na msisimko¿‽```Wiki hii tujifunze dalili _zifananazo_ Kati ya Upendo💖 na msisimko🔥.

 *1.MHEMKO* : Hisia kali za ngono kwa mtu wa jinsia tofauti.Wanaume hukutwa na hali hii kwa kasi kuliko wanawake .Mihemko mikali ya ngono haumaanishi 💖.Hali hii hutokea kotekote katika 💖 na 🔥. Msisimko ni hatua yenye nguvu-mno(intense) kiasi kwamba haiwezi kudumu mda mrefu.Hakuna binti/kijana awezaye kuvumilia nguvu hii , hata wakiapiana kudumusha hali hii.Mara nyingi hali ya 🔥ikidumu sana ni miezi 3 hadi 6. _lkitokea Wakaoana , msisimko ukiisha watagundua hakuna kitu kingine kilichobaki kuwaunganisha_ .

 *2.SHAUKU YA KUWA PAMOJA*: Shauku ya kuwa karibu iko katika 💖 halisi ulivyo katika🔥.Waweza kutamani kukaa na mwenzio MUDA WOTE , ukawa unahofu kubwa bale inapobidi kutengana.Unaweza  kujihisi mpweke na mtupu( empty) pale ambapo haipo Nate , lakini hii haumaanishi una upendo wa kweli.

 *3.HISIA ZA NGENI:* Katika 🔥Kama ilivyo katika 💖 , unaweza kuhisi hisia ngeni na za kushangaza. Mambo yakikunyookea Waweza kuhisi Kama unatembea hewani 🧚🏽‍♂️na ukahisi kugonjeka mambo yanapokwenda mrama. Hisia hizi hudhihirika zaidi katika 🔥kuliko katika💖.Tena mhusika hupoteza uwezo wa kujitawala na kujizuia..... Uzoefu fulani ulio/unaopitia   unaweza kukufanya Uwe mwenye kuathiriwa kirahisi (vulnerable) na msisimko🔥.Mfano; unapokuwa mpweke au wakati ukiombolezea mahusiano yaliyovunjika , katika hali Kama hii ni rahisi kutafsiri mahusiano mapya Kama 💖wa kweli kumbe yaweza kuwa yaleyale🔥.

 ```Sasa nitawezaje kutofautisha Kati ya Upendo halisi💖na Msisimko``` 🔥 *¿‽....Yajayo yanafurahisha*







*PMC 360°©2021™*

No comments