Kikubwa zaidi nilichojifunza kwenye kitabu cha Mzee Mwinyi ni kwamba Mzee Mwinyi ni Baba wa Mageuzi, alipoingia madarakani Nchi yetu ilikuwa vibaya kiuchumi lakini alipoingia akafanya mageuzi, alianzisha ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ikiwemo Kiwanda cha Bia.
Mzee Mwinyi anasema alibinafsisha Kiwanda cha Bia Tanzania kwasababu kilikuwa kinaendeshwa kwa hasara, kabla ulikuwa ukitaka bia kwa ajili ya harusi ilikulazimu kupata kibali cha kununua bia kutoka kiwandani au kwa Wakala tena kwa kuonesha kadi za mialiko ya harusi” Rais SSH.
0 Comments