Serikali imepanga kuweka utaratibu wa kutambua hatua mbalimbali za upatikanaji wa nyavu za uvuvi tangu kutengenezwa kwake hadi kusambazwa na kumfikia mvuvi ili kudhibiti usambaaji wa nyavu zisizohitajika kisheria hapa nchini.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo (22.05.2021) wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kanyala kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo na kubainisha kuwa serikali inataka suala la kuchoma nyavu lipungue au liishe kabisa.
“Tumejipanga vyema sana wavuvi mmekuwa mkipata sintofahamu kubwa unaenda dukani kununua nyavu ya milimita nane (8) ukija nayo huku ikipimwa inaonekana iko chini ya milimita hizo ambapo ni kinyume na sheria na wewe kuchukuliwa hatua, sasa tutapambana na wauzaji na wasambazaji wa nyavu hizo.” Amesema Mhe. Ulega
Ameongeza kuwa ili kuhakikisha nyavu za uvuvi zinakuwa katika viwango vinavyotambulika, wizara itaweka pia utaratibu wa kuwepo kipimo kimoja ambacho kitatambulika nchi nzima kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kumuokoa mvuvi asiendelee kuumizwa kwa kuarifiwa kuwa nyavu zake ziko kinyume na sheria.

0 Comments