Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDARI YA MAGAPWANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Magapwani na kueleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa maamuzi yenye tija kwa ajili ya muendelezo wa eneo hilo.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo, mara baada ya kufanya ziara ya kulitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Mangapwani, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo pia, alitembelea miradi ambayo imeanza kabla ya ujenzi huo mpya.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali itakuja na maamuzi yenye tija ambayo yatasaidia kwa pande zote mbili ikiwemo upande wa wawekezaji ambao walianza kuekeza kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na kwa upande wa Serikali kwa ujumla huku akiwataka wawekezaji hao kuwa na subira .

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali imeridhishwa na ukubwa wa eneo pamoja na hatua ya awali iliyofikiwa na kueleza jambo kubwa lililompelekea kufanya ziara hiyo hivi leo ikiwa ni kwenda kujiridhisha na kulielewa vyema eneo hilo.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwasisitiza wawekezaji hao kuwa na subira huku akisema kwamba atahakikisha jambo hilo linakwenda kwa haraka na ameahidi kukaa na wahusika mapema iwezekanavyo kwa azma hiyo hiyo ya kuharakisha mradi huo.

Alitumia fusra hiyo kutoa shukurani kwa wananchi wa eneo hilo kwa utayari wao waliouonesha kwa kuruhusu maendeleo kwa kushirikiana na Serikali yao kwa kuupisha mradi huo mkubwa wa bandari.

Post a Comment

0 Comments