Advertisement

Responsive Advertisement

MYANMAR KWENYE MASHINDANO YA MISS UNIVERSE

Thuzar Wint Lwin, ambaye alishika nafasi ya 21 bora katika mashindano hayo, alitumia siku zilizotangulia fainali kwa kuweka angalizo juu ya mapinduzi nchini mwake. ⁠
"Watu wetu wanakufa na kupigwa risasi na jeshi kila siku," alisema wakati wa video yake ya wasifu, ambayo ilionyesha picha zake akishiriki katika maandamano ya kupinga mapinduzi. "Kwa hivyo ningependa kusisitiza kila mtu azungumze juu ya Myanmar."
Alishinda pia tuzo ya vazi bora la kitaifa. 

Alivaa mavazi yenye shanga katika mifumo ya jadi ya Kiburma na alishikilia ishara iliyosema: "Ombeni Myanmar".

Post a Comment

0 Comments