Kama ni kweli hii sauti inayosika hapa ni ya Meneja au Wakala wa Meddie Kagere basi huyo jamaa hana weledi kabisa. Simba ina wachezaji wengi ambao hawapati nafasi ya kucheza kama ambavyo wangependa au mawakala na mameneja wao wangependa.
Lakini wanavumilia ili kuheshimu maamuzi ya Kocha lakini kuwapa heshima stahiki wachezaji wengine wanaocheza ambao ni wa Simba pia na wana haki kama walivyo wengine.
Sasa kuanza kuhusisha mambo binafsi au tofauti zenu binafsi kwenye biashara na kuziweka hadharani sidhani kama ni sawasawa. Hii inaharibu sifa na heshima ya Klabu, Kocha na Kagere kwa pamoja.
Bocco kwa mfano ni Nahodha wa Simba ambaye amekuwa na kipindi kigumu tangu ujio wa Kocha Gomez ukilinganisha na wakati wa Sven, mbona hatujamsikia Meneja au Wakala wake wakilalama kama hivi?
Lakini Waandishi wa habari wanamhoji Wakala au Meneja juu ya kwanini mchezaji wake hakucheza mechi...? Kwanini asihojiwe Kocha ambaye ndiye anafanya nao mazoezi na ana amua nani acheze na nani asicheze! Kwahiyo Waandishi hawajui jukumu la Kocha na lile la Meneja/Wakala wa mchezaji?
Kama hii sauti sio kweli kwamba ni Meneja/Wakala wa Kagere, Simba na Kagere wangeikanusha hii kitu haijakaa vizuri. Kama ni kweli, Simba na Kagere waongee nae ili amuombe radhi Kocha, Klabu, Wachezaji na Wanasimba wote.

0 Comments