Advertisement

Responsive Advertisement

MAFUNZO YA WATU WAZIMA LEO 27

LESONI, MEI 27

SOMO: AHADI YA MASIHI: SEHEMU YA KWANZA 



“Na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 28:14). 

“Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi” (Gal. 3:29)



Zaidi ya mara moja BWANA alimwambia Ibrahimu kuwa kupitia uzao wake, mataifa yote ya dunia yatabarikiwa (soma #Mwanzo 12:3,# #Mwanzo 18:18,# #Mwanzo 22:18#). Ahadi hii ya agano imerudiwa, kwa sababu miongoni mwa ahadi zote hii ndiyo muhimu zaidi, yenye kuhimili kwa muda mrefu, inayofanya ahadi zote zingine ziwe na maana. Kwa namna moja, hii ndiyo ahadi ya kuinuka kwa taifa la Kiyahudi, ambalo kupitia kwake BWANA alitaka kufundisha “jamaa zote za dunia” kuhusu Mungu wa kweli na mpango wake wa ukombozi. Hata hivyo, ahadi hizo hufikia utimilifu wake katika Yesu Kristo, ambaye ametoka kwenye uzao wa Ibrahimu, ambaye pale msalabani atalipa bei kwa ajili ya dhambi za “jamaa zote za dunia.” 



Tafakari ahadi ya agano iliyofanyika baada ya Gharika (ambapo BWANA anaahidi kuwa hataangamiza tena dunia kwa maji). Je ahadi hii itakuwa na faida gani pasipo ahadi ya ukombozi upatikanao katika Yesu? Ahadi za Mungu zitakuwa na faida gani pasipo ahadi ya uzima wa milele upatikanao katika Kristo? 



Je unaelewaje kauli kuwa ndani ya Ibrahimu, kupitia Yesu, “familia zote za dunia” zitabarikiwa? Je hiyo humaanisha nini?



Naam, ahadi ya agano kuhusu Mwokozi wa dunia ndiyo ahadi kuu miongoni mwa ahadi zote za Mungu. Mkombozi Mwenyewe anakuwa njia ambayo kwayo masharti ya agano yametekelezwa na ahadi zake zote zingine zinafanikiwa. Wote, Wayahudi na Wayunani, na wale ambao huingia katika uhusiano naye kwa imani huhesabiwa kama wanafamilia halisi na warithi wa ahadi (#Gal. 3:8, 9, 27—29#), yaani —ahadi ya uzima wa milele katika mazingira safi ambapo uovu, maumivu na mateso havitainuka tena. Je, waweza kufikiria ahadi bora kuliko hiyo?



Je ahadi ya uzima wa milele katika mazingira yasiyo na dhambi wala mateso hukupatia hamasa gani? Je hiyo ni shauku yetu kwa vile hapo mwanzo tuliumbwa kwa kusudi hilo na kwa kujawa shauku kuurithi tunatamani kitu ambacho ni cha msingi kulingana na asili yetu?




Post a Comment

0 Comments