Advertisement

Responsive Advertisement

HUSSEIN MWINYI AZIPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI ZA INDIA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amezipongeza juhudi za Serikali ya India za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za kiuchumi na kijamii
 
Rais Dk Mwinyi aliyasema hayo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa India anayefanyia kazi zake hapa Zanzibar Bhagwant Singh.
 
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na India ambao umeipelekea nchi hiyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza miradi yake ya maendeleo.
 
Katika maelezo hayo, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya India kwa kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo, biashara, huduma za jamii, uendelezaji wa rasilimali watu na nyenginezo.
 
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza azma ya Serikali ya India ya ujenzi wa chuo cha amali huko kisiwani Pemba ambacho kitatoa mafunzo ya utalii pamoja na usarifu wa vyakula mbali mbali.
 
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo ya Serikali ya kukuza ajira kwa vijana pamoja na kuifanya Pemba kuwa ni sehemu maalum ya uekeza sambamba na kuweza kutoa mafunzo kwa vijana katika kuendeleza sekta maendeleo ikiwemo utalii.
 
Rais Dk. Mwinyi pia, alizipongeza juhudi za Serikali ya India za kuuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za maji safi na salama.

Post a Comment

0 Comments