Advertisement

Responsive Advertisement

ANAANDIKA MWIJAKU

Siku zote, ua lililopo bustanini hua halifikirii kushindana na Ua lenzake lililopo jirani. Yote huchanua. Usijihisi vibaya endapo utakataliwa.

Siku zote watu huacha vitu vyenye thamani kwa sababu wameshindwa kuvi-afford.

Kama umefanya makosa, inamaanisha kuna nafasi ya kurekebisha na kuanza upya. Sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, ila ufunguo wa kufeli ni kum-please kila mtu na kukubali kuwa mtumwa wa mawazo yake.

Kiwango cha juu cha hekima ni kuishi sasa, kupanga ya baadae na kufaidika na jana yako. Nimejifunza kwamba, mtu jasiri sio yule asiyeogopa lolote, bali ni yule anayeushinda uoga wake ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi magumu.

Naam, maamuzi magumu yenye tija katika maisha. Nikutakie Jumatatu Njema!

Post a Comment

0 Comments