Advertisement

Responsive Advertisement

MAMBO 10 NA ALI KAMWE

MAMBO 10 NA ALI KAMWE "YANGA SC 3 -1 GWAMBINA FC" ✍

Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Gwambina

1: Another Day. Another Match. Anothor Win kwa YANGA. Wananchi wameondoka na Pointi 3 zingine za thamani kuelekea kwenye mbio za Ubingwa🙌

2: Gwambina walikuja na 'Game Plan chafu'  ili kujaribu kutengeneza presha kwa Yanga majukwaani ili wapate faida yao kiwanjani. Kivipi?

3: Tangu dakika ya kwanza walilazimisha mechi iwe na tempo ya chini. Waliamini ingetengeneza presha kwa mashabiki kuja kiwanjani. Wachezaji wangepaniki na kupunguza ufanisi wao. Bahati mbaya, Yanga wana wachezaji wakubwa wakuishi katika presha na kutumia nafasi. Wakawaadhibu kikatili.

4: Juma Mwambusi alikuja na system ya 4-1-4-1 akinufaika na uwezo wa Carlinhos na Mukoko namna walivyokuwa wakiswitch katika Transition mbili (Kukaba na kushambulia)

5: CARLINHOS 🙌 WoW. What A player. 'Brain' yake kwenye kutafuta nafasi huru kupokea pasi na vision yake kwenye kuipiga kwenye nafasi sahihi iliwatesa sana Gwambina. He was so Good namna alivyokuwa akicheza kama 'Deep Play Maker'. 

6: Kitendo cha Ntibazonkiza ni ishara kuwa Timu ilishakuwa juu ya mabega ya Mwambusi. Nidhamu Zero. Kambi ina makundi na 'uspesho' wa kipuuzi. No wonder Timu ilikuwa inapata shida kiwanjani. Mashabiki wanaumia bila sababu. Wachezaji kama wameshindwa kuheshimiana, walitakiwa kuheshimu Logo ya Klabu kwenye jezi wanazovaa. 

7: Gustavo Simon 🙌 Asante kwa kipaji chako. Dhidi ya Tuisila, alisimama na kuibuka mbabe. Hakutaka kukimbizana, yeye alikaba nafasi tu. Safi sana👏

8: NINJA🙌 Kazi aliyotumwa aliifanya kwa 100%. Nonga hakutema wala kumeza. Thats Very Good kwenye jukumu hilo. Lakini bado ana mengi ya kuboresha kwenye utulivu wake pindi timu inapokuwa na mpira. Eneo analocheza, pasi moja mbovu ni risk kwa timu.

9: Meshack Abraham, Yusuf Dunia. Siku nyingine mbovu kwao dhidi ya Timu kubwa. Confidence yao hushuka. Hucheza kwa kupania mno kuliko kutumia 'quality' zao

10: Hongera Nchimbi. Safi sana. Bao zuri katika siku nzuri kocha mpya akiwa jukwaani. Napenda mabadiliko ya Kibwana Shomari. Angalau ameanza kuzoea kusogea. Kazi iliyobaki ni kuboresha krosi yake tu kwenye boksi

Nb: Kwa timu ile, Mwarabu asipange nguo zote kabatini😀

Post a Comment

0 Comments