Kaizer Chiefs wamewaangusha vigogo, Mamelodi Sundowns baada ya kuwachapa 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Afrika Kusini leo.
Huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa Mamelodi Sundowns kupoteza msimu huu na kwa ushindi huo, Kaizer Chiefs inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 22 na kupanda kwa nafasi tano hadi ya 8
Pamoja na kufungwa, Mamelodi Sundowns inayobaki na pointi zake 47 baada ya kucheza mechi 22 sasa, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Amazulu ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili zaidi.
Wafungaji: (Sirino 35’) Mamelodi Sundowns 1 : 2 Kaizer Chiefs (Lebusa o.g 72’, Zuma 74)
0 Comments