Mbunge wa Makambako (CCM), Deo Sanga ametaka tabia ya baadhi ya wabunge na viongozi wastaafu kusemwa vibaya katika mitandao ya kijamii akiwemo rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kukomeshwa kwa maelezo kuwa ikiachwa itaibua sintofahamu nchini.
Sanga maarufu Jah People ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 21, 2021 katika mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2021/22.
Mbali na Kikwete, amesema wengine wanaosimangwa mitandaoni ni mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, katibu mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
“Nani atafuata mheshimiwa Spika hii ni hatari, ni lazima tukemee kwa jambo ambalo linaweza kutugombanisha Watanzania. Hayo ni hatari kwa vitu ambavyo wameandika kule. Tukiliacha likaendelea kesho kutwa hatujui atawekwa nani.”
“Mheshimiwa Kikwete akapumzike amefanya kazi yake vizuri, Kinana akapumzike. Nape wewe ni shahidi 2013 hadi 2015 wakati wa uchaguzi..., Nape na Kinana walizunguka miaka mitatu kutafuta kura za CCM,” amesema.
Amebainisha kuwa katika kutafuta kura hizo Nape alikatwa hadi kiganja na Kinana kupata maumivu ya bega.
“Na wewe (Ndugai) wameanza kukuweka katika mtandao, wakuache ufanye kazi yako vizuri. Suala la Bagamoyo (bandari) Spika alichokisema ni nini? Amesema lijadiliwe. Nyinyi mna uwezo wa kusema hiki kinafaa hakifai,” amesema.
Baada ya kumaliza mchango huo, Ndugai amesema, “Nilimvumilia maana seneta ndio wazee wa mji huu
0 Comments