*KESHA LA ASUBUHI*
Alhamisi, 22/04/2021
*MAAGIZO KWA AJILI YA UMOJA.*
*Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu*.
*Mathayo 6 :14, 15*
Kuna jambo ninatamani kuzungumza nawe juu ya unavyojisikia juu ya Ndugu A. Upo katika hatari ya kuwa mkali sana kutokana na maumivu aliyokusababishia. Lakini kaka yangu, kama kweli amekukosea wewe, je huwezi kuona kuwa yeye ndiye anayeumia na siyo wewe? Nina uhakika unatakiwa kuonesha uungwana wa Kikristo katika suala hili, msamehe na usiruhusu mafarakano yoyote.
Je! ndugu yangu atakumbuka deni lake kubwa kwa BWANA na ni kwa kiasi gani anahitaji msamaha, huruma na upendo Wake? *Je! atakumbuka kuwa... kama hutamsamehe ndugu yako makosa yake, wala Baba yako wa mbinguni hatakusamehe makosa yako? (Tazama Mathayo 6:15)*.
Je utatumia ujuzi wako kufanya yote yaliyo ndani ya uwezo wako kuwa na umoja na Ndugu A? Hebu mwandikie kama ndugu. *Vunja kila kikwazo na kusiwe na utofauti kati yenu. Mpendane kama ndugu, wenye huruma na kuheshimiana. Ninapendekeza kwenu upendo wa Kristo utumike kwa kiasi kikubwa utaleta mabadiliko makubwa kwani una nguvu ya ajabu ya kuponya*.
*Hufikirii kuwa mbingu yote itawatazama kwa furaha kama utafungua moyo wako kwa upendo wa Kristo wenye huruma? Mzee A atalitafakari hili suala na hivyo nawe pia kadiri tofauti hizi zinaendelea kuwepo na kukuzwa kati yenu. Lakini *hebu kila mzizi wa uchungu ung’olewe na kuzikwa*.
Inawezekana kuwa una mtazamo mbaya kwa dhamira halisi ya Mzee A. Na pia unaweza ukawaza, kuongea na kujisikia zaidi ya ambavyo ungejisikia na unamwelewa vibaya ndugu yako.
*Shetani atapendezwa sana kwa ninyi kuwa na roho ya kutokusamehe badala ya kurejeresha uhusiano wa karibu. Lakini Yesu aliyeweka thamani kuu kwa mwanadamu, anaumizwa kuona utengano miongoni mwa ndugu. Ninatamani wote tungekuwa kama Yesu alivyotoa kielelezo kwa maisha yake. Alikuja ili kuokoa maisha ya watu siyo kuangamiza. Alitumia uwezo wake kubariki na si kuumiza. Maneno, uvumilivu na kazi zake zilijaa rehema za Kiungu. Hakuna ambacho kingeharibu ustahimilivu wake au kumchochea kutosamehe. —Letter 46, April 22, 1887, to Dr. J. H. Kellogg.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
0 Comments